Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, September 2, 2013

Kapombe azuiwa kutembea Ufaransa


Mchezaji wa AS Cannes, Shomari Kapombe.
Na Mwandishi Wetu
KITENGO cha afya cha Klabu ya AS Cannes, kimemtaka mchezaji wake mpya, Shomari Kapombe, kutulia ndani muda mwingi na kuepusha kutembea bila sababu za msingi.
Uamuzi huo unatokana na kutaka kuona Kapombe anapona haraka na kurejea dimbani kwa ajili ya kuichezea timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ufaransa.
Jean Pierre, mmoja wa wauguzi wanaofanya kazi katika kitengo cha tiba cha timu hiyo, amesema jana kwamba Kapombe anaendelea vizuri.
 “Matumaini yetu ni apone haraka na kurudi uwanjani. Tumempa siku kumi na tano za kupumzika kutokana na tatizo hilo la kidole.
“Lakini lazima apumzike, tumemtaka ahakikishe hatembei bila kuwa na sababu za msingi. Aupumzishe mguu kwa muda mwingi ili apone haraka.
“Tuna wachezaji wengine watatu katika kikosi chetu ambao ni wagonjwa pia, tumekuwa na utaratibu wa kuwafuatilia kwa ukaribu kabisa na kama Kapombe atapona haraka, ataanza mazoezi ya taratibu kabla ya kujiunga na wenzake mazoezini,” alisema Pierre juzi mchana.
Wiki iliyopita, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen, alitangaza Kapombe hatajiunga na kikosi chake pamoja na kuwa amemuita na hali hiyo inatokana na kufanyiwa upasuaji wa kidole cha mguu.
Kapombe amejiunga na timu hiyo akitokea Simba ambayo aliichezea kwa mafanikio makubwa.CHANZO GPL

No comments:

Post a Comment