Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
kati ya Simba na Mgambo Shooting Stars iliyochezwa jana (Septemba 18
mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh.
58,365,000.
Watazamaji 10,241 walikata tiketi
kushuhudia mechi hiyo namba 23 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika
kwa wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa mabao 6-0.
Viingilio katika mechi hiyo
vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 13,839,327.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 8,903,135.59.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 7,036,946.16, tiketi sh. 2,548,890, gharama za
mechi sh. 4,222,167.70, Kamati ya Ligi sh. 4,222,167.70, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,111,083.85 na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,641,954.10.
MIKATABA YA MAKOCHA VPL, FDL YATAKIWA TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limetoa siku 14 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na
za Ligi ya Daraja la Kwanza (FDL) kuwasilisha mikataba ya makocha wao.
Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya TFF iliyokutana Septemba 12 mwaka huu imebaini klabu nyingi
hazijawasilisha mikataba ya mabenchi yao ya ufundi, kitu ambacho ni
matakwa ya kikanuni. Siku hizo 14 zimetolewa kuanzia Septemba 17 mwaka
huu.
Kwa klabu ambazo zitashindwa
kuwasilisha mikataba hiyo na vielelezo vingine ndani ya mudau huo
zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment