Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, September 22, 2013

Taribo West, Keshi waporwa mali


NFF1 46e8f
SUPASTAA wa zamani wa Nigeria, Taribo West na kocha wa sasa timu ya taifa ya nchi hiyo, Stephen Keshi, wameripotiwa kuporwa ardhi waliyopewa kama zawadi baada ya kuisaidia Super Eagles kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2002 zilizofanyika Japan na Korea Kusini. (HM)

Wawili hao sambamba na wachezaji wengine waliokuwa wakiunda Super Eagles waligawiwa vipande vya ardhi katika eneo la Port Harcourt, kusini mwa Nigeria na gavana wa zamani wa Rivers State, Peter Odili.
west eea2e
Hata hivyo, kwa mujibu wa West maeneo hayo yameporwa na wavamizi na aligundua hilo baada ya kwenda kwenye ardhi yake akitaka kuanza kuiendeleza.
"Nilikwenda kwenye eneo langu na kukuta limechukuliwa na wavamizi. Si mimi pekee, kuna wachezaji wengi akiwamo Keshi maeneo yao yamechukuliwa pia," alisema West huku akionyesha kuchukizwa na jambo hilo. West alichezea Nigeria mechi 41 kati ya 1994 na 2002. Chanzo: mwanaspoti

No comments:

Post a Comment