Waziri
Mkuu Mizengo Pinda (katikati), akiitembeza na kuionyesha timu ya
Serengeti Fiesta baadhi ya vitu vinavyofanyika shambani hapo.





TIMU
ya Serengeti Fiesta hususani iliyoupande wa kampeni ya Kamata Fursa
Twenzetu, jana ilipata mwaliko kutoka kwa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo
Peter Pinda wa kutembelea katika mashamba yake.
Timu
hiyo ilifika kwenye mashamba hayo yaliyopo Kizota nje kidogo ya mji wa
Dodoma eneo la Zuzu ambalo ndilo jina halisi la mashamba hayo
yanayohusika na shughuli mbalimbali za kilimo, ikiwemo ufugaji wa mbuzi
zaidi ya mia mbili, kilimo cha zabibu, nyanya, ndizi na ufugaji wa
asali.
Timu hiyo ilikuwa ikiongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi, Uzalishaji na
Mipango wa Clouds Media Group, Rugemalila Mutahaba ‘Ruge’, ilipata fursa
ya kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa Waziri Mkuu, hasa kuhusiana na
namna ya kutumia fursa ya kujikwamua kimaisha kupitia kilimo na
ufugaji.
(HABARI/PICHA:MUSA MATEJA/GPL)
P
No comments:
Post a Comment