skip to main |
skip to sidebar
WAZIRI DK. NCHIMBI AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI HOSPITALI YA MUHIMBILI LEO
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba
wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika
Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kumpa pole, baada ya
kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa
wa Mjini Magharibi, Zanzibar wiki iliyopita. Dk Nchimbi alimtoa hofu
Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa, na
serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi chochote
kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya
tindikali. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi (kushoto) akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la
Romani Katoliki Parokia ya Machui, akitoa maelezo jinsi alivyopata
mkasa wa kutiwa Tindikali na watu wasiojulikana, Mjini Unguja, Zanzibar
alipofika katika Hospitali ya Muhimbili kumpa pole, ambapo amelazwa na
kuapatiwa matibabu. Dk Nchimbi alimtoa hofu Padri huyo akimuahakikishia
kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa, na serikali itapambana
kikamilifu na mtu au kikundi chochote kitakachojihusisha na vitendo vya
uhalifu wa kutumia kemikali ya tindikali. Picha na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi (kushoto) akimuhakikishia Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa
la Romani Katoliki Parokia ya Machui, Zanzibar jinsi wizara yake
itakavyopambana kwa kuwakamata wale wote watakaojihusisha na vitendo vya
uhalifu wa kutimia kemikali ya tindikali. Dk Nchimbi alifika
hospitalini. Dk Nchimbi alifika katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar
es Salaam kumpa pole padri huyo ambaye anatarajiwa kupelekwa nchini
India kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.Hata hivyo,Dk Nchimbi alimtoa
hofu Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa,
na serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi chochote
kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya
tindikaliPicha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.(
No comments:
Post a Comment