Barcelona itameyana na wenyeji wao hao, Milan kwenye Uwanja wa San Siro Jumanne usiku, lakini nyota kama Neymar, Alex Song na Dani Alves walionekana kupendeza zaidi baada ya kutua Italia.
Wakiwa wamepigilia shati kali, suti za nguvu na miwani ya jua, watatu hao walifunika mbaya kiasi cha kuonekana kama nyota wa filamu wakati kikosi cha timu ya Katalunya kinatua mjini humo.
Safari kutoka Barcelona hadi Milan inawakutanisha tena wachezaji wa timu hizo kutokana na timu hizo mbili kuwa zimekutana mara sita katika misimu miwili iliyopita huku Barca wakiongoza kupata matokeo mazuri na kuitoa Milan katika Ligi ya Mabingwa mara mbili.
Barca inaingia kwenye mchezo wa kesho ikiwa haijapoteza pointi wala kuruhusu hata nyavu zake kuguswa kwenye mechi za Kundi H, lenye timu za Celtic na Ajax pia.
Milan kwa sasa wapo katika mwanzo mgumu katika ligi ya kwao, Serie A wakiwa wameachwa kwa pointi 13 na vinara AS Roma.
Timu hiyo ya Italia pia inakabiliwa na janga la majeruhi, kipa Christian Abbiati, beki Daniele Bonera na washambuliaji Stephan El Shaarawy, Mario Balotelli na Giampaolo Pazzini wapo katika chumba cha matibabu.
No comments:
Post a Comment