Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Asangye Bangu
akiongea na waandishi wa habari Wakati wa kutangaza kuanza kutumika kwa
Huduma ya M-pesa kukusanyia marejesho ya mikopo kwa wanufaika wa bodi
hiyo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na
Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi Juma Chagonja
"Tunayofuraha kubwa sana leo kutangaza
kwamba sasa wanufaika wa mikopo ya Bodi wanauwezo wa kutumia mfumo wa
M-pesa kufanya marejesho ya mikopo yao moja kwa moja kwa Bodi."Alisema
Bangu
Bingu
amesema bodi inaimani kuwa M-pesa itawapatia urahisi wanufaika kuweza
kutimiza wajibu wao kisheria wa kurudisha mikopo waliopatiwa kwa ajili
ya masomo ya elimu ya juu.
Amesema
wanufaika wa mikopo wanapaswa kuanza kurejesha mikopo yao mara baada ya
miezi 12 kuanzia wanapohitimu masomo ya elimu ya juu au wanapositisha
masomo kwa sababu yoyote ile, akiwa ameajiriwa ama hajaajiriwa.
Bingu
amesema wanufaika walioajiriwa wanalipa mikopo yao kupitia kwa waajiri
wao ambapo hukatwa marejesho ya mikopo kwenye mishahara yao ya kila
mwezi na mwajiri huwasilisha makato hayo kwenye Bodi kupitia kwenye
akaunti zake huku wale ambao sio waajiriwa hupeleka huwasilisha
marejesho ya mikopo katika benki za bodi.
"Wanufaika
wanaorejesha mikopo yao kwa pesa taslim wamekuwa wakipata changamoto
mbalimbali wakati wa urejeshwaji wa mikopo yao kupitia kwenye akaunti za
Benki ikiwa ni na benki hizo kutokuwa na matawi ya kutosha yaliyokaribu
na warejeshaji wa mikopo pamoja na kutumia muda mwingi kwenye
foleni."Alisema Bingu "M-pesa itapunguza changamoto hizo na hatimae
kuwajengea mazingira mazuri ya urejeshwaji wa mikopo, Bodi inatangaza
rasmi kuanza kutumika kwa utaratibu huu mpya wa urejeshaji kwa M-pesa
kuanzia sasa."
Kwa
upande wake Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Bw. Salum Mwalim amesema
kuzimduliwa kwa huduma hiyo ni mwendelezo wa jinsi ambayo huduma ya
M-pesa inavyorahisha miamala nchini kuzidi kuwa rahisi.
"M-pesa
imekuwa suluhisho la changamoto nyingi zinazohusiana na malipo ama
miamala mengine ya kijamii na kibiashara."Alisema Mwalim na kuongeza.
"Ni wazi sasa hakuna atakaekuwa na usumbufu katika kulipia mkopo wake
kwenye Bodi ni kiasi tu cha kupiga *150*00# na hapo anauwezo wa kufanya
mrejesho wake wakati wowote mahali popote."
"Tunaishukuru
Bodi kwa kuendelea kuiamini huduma yetu ya M-pesa walianza kwa kuitumia
katika ukusanyaji wa ada za uombaji wa mikopo na sasa wanakwenda mbali
zaidi kwa kuichagua kuitumia katika makusnayo ya marejesho ya mikopo
kutoka kwa wanufaika."Aliongeza
Mwalim
amesema kwa njia hiyo ni wazi sasa Bodi itashuhudia mabadiliko makubwa
kwenye makusanyo ya marejesho kwa kuwa huduma hiyo imeenea nchi nzima na
hasa kwa kuwa inauwezo pia wa kumuunganisha mteja na benki yake.
"Kwa
mtandao mpana wa huduma hii mawakala na na mtengamano wake na mabenki na
jinsi inavyotumika ni wazi mtarajie ufanisi kwa kuwa sasa mmewawezesah
wanufaika wa mikopo kuwa na uwezo wa kufanya marejesho kwa njia rahisi
zaidi Wakati wowote mahali popote kwa usalama na uhakika
zaidi."AAliongeza
Ili
mnufaika aweze kulipia kupitia M-pesa anapaswa kwanza kuhakikisha kuwa
ana taairfa ya Mkpo(loan Statement),Kiwango cha Marejesho na Nambari ya
Kumbukumbu amabvyo vinapatikana ofisi za Bodi hiyo ya mikopo. Taarifa
hizo zitatumika Wakati w akulipia baada ya mteja kupiga *150*00# kutoka
kwenye simu yake ya Vodacom na kuchagua nambari nne ambayo ni ya malipo
na kuendelea na maelekezo kadri yanatakavyokuwa akiyapata kutoka kwenye
simu yake ya kiganjani
No comments:
Post a Comment