Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 17, 2013

Dereva tax achinjwa na abiria

 

 

DEREVA tax mkazi wa Chalinze Mohamed Mrisho (27) ameuawa kikatili kwa kukatwa shingo na kutenganishwa na kiwiliwili cha mwili huko kijiji cha Bago kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo
Watuhumiwa wa tukio hilo wametajwa kuwa ni watu wawili wa kiume ambao walifika majira ya saa 1.15 usiku kituoni Chalinze kisha kumtaka dereva huyo awasafirishe kwenda kata ya  Kiwangwa wilayani humo.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei amethibitisha tukio hilo ambapo  amesema limetokea majira ya saa moja usiku wa kuamkia jana wakati dereva huyo akiwa katika shughuli zake za kusubiri wateja wa huduma hiyo ya tax.
Matei amesema tayari mtuhumiwa mmoja aliyemtaja Peter Charles (21) anashikiliwa na jeshi hilo huku mwenzake aliyetajwa jina moja la John akiendelea kusakwa.
Matei amesema ametaja gari walilolikodi watuhumiwa hao ni T 426 BUT aina ya Avenlit na lilikuwa linaendeshwa na marehemu huyo.
 
Aliongeza kuwa abiria hao walitembea na hilo gari lakini hawakufika nalo mbali kwani walipata ajali na kutumbukia mtaroni huko Msata.
Kamanda huyo amesema kama ilivyo ada ikitokea ajali watu hujitokeza kusaidia na ndivyo ilivyokuwa kwa watuhumiwa hao wananchi walifika kutoa msaada lakini walipokaribia karibu mmoja wa watuhumiwa aliyetajwa jina moja la John alikimbia na hivyo walimkamata Peter na walipomuhoji walibaini si mali yao hivyo kutoa taarifa Polisi.
Amesema askari walifika eneo la ajali na kufanya upekuzi ambapo walikuta kisu yenye damu ndani ya gari na kumuhoji mtuhumiwa ambapo aliwapeleka askari hao eneo walikofanyia mauji na kukutwa mwili wa marehemu pembeni mwa barabara na pembeni mwake kulikutwa pia kisu kingine kilichotapakaa damu.
 Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi wa daktari kisha kukabithiwa ndugu kwa mazishi.

No comments:

Post a Comment