Dk Slaa aliwasili nchini Marekani tarehe 21 Septemba 2013 akiambatana na mkewe mama Josephine Mushumbuzi na kupokelewa na Uongozi wa Chadema DMV.
Tarehe 22 Septemba 2013 Dr Slaa alifanya mkutano uliojumuisha wanajumuia ya Watanzania waishio katika Majimbo ya Washington, Maryland na Virginia.
Katika ziara yake Dk Slaa alitembelea
majimbo ya North Carolina na Alabama ambako alitembelea Vyuo Vikuu na
Taasisi mbalimbali na kujifunza Shuguli nyingi za Maendeleo katika Sekta
mbalimbali ikiwemo Kilimo, Afya, Nishati na Uchumi.
Akizungumza akiwa uwanja wa Ndege wa Dulles mjini Washington Dk Slaa alisema alichojifunza akiwa Marekani anatarajia kupeleka maarifa hayo Tanzania ili yaweze kumkomboa Mtanzania kutoka katika Umaskini. Moja katika mambo ambayo amejifunza ni namna ya kutumia nishati ya Jua kuzalisha umeme hasa kwa wakazi wa Vijijini.
Dk Slaa amekamilisha ziara yake ya wiki tatu nchini Marekani iliyopewa jina la "Vision Tanzania" baada ya kualikwa na Umoja wa Vyuo vikuu nchini Marekani.
Taarifa hii imetolewa na waratibu wa CHADEMA Blogs

No comments:
Post a Comment