Mke wa
rais mama Salma Kikwete katikati akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr
Christine Ishengoma leo kabla ya kuzindua jengo la huduma ya wanawake na
watoto katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Mfanyabiashara
Salim Asas Abri katikati ambae ni mmoja kati ya wadau wakubwa wa
uchangiaji wa maendeleo ya mkoa wa Irionga akiwa katika ufunguzi wa
jengo hilo
Dr.Manyama mwenye tai akiwa na wadau wengine wakisimsikiliza Mama Salma Kikwete
MKE wa Rais mama salma Kikwete amezindua wodi la kisasa la huduma ya wanawake na watoto katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa huku akipongeza jitihada kubwa zilizofanyika katika Hospital hiyo katika kuboresha huduma ya mama na mtoto.
Mbali ya kuzindua jengo hilo bado mama
Salma Kikwete amewashukia wakazi wa mkoa wa Iringa ambao wanaendelea
kuongeza kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa kusaliti ndoa zao
na kuwataka kuacha mara moja.
Akifungua wodi hilo leo Mama Kikwete alisema kuwa serikali imelenga kuendelea kuboresha huduma ya afya na kuwa mbali ya kuboresha majengo bado serikali imeendelea kuboresha elimu ya watoa huduma kama njia ya kuboresha zaidi huduma ya afya.
Hata hivyo alisema changamoto za madawa na madaktari serikali itaendelea kushughulika na kuwataka wanawake kuendelea kutumia majengo hayo na kuepuka kuwapeleka watoto kwa waganga wa kienyeji ama wao kujifungulia majumbani .
Kwani alisema kukamilika na kuboreshwa kwa huduma hizo ni kuepusha wazazi na watoto kuendelea kuwa na fikra potofu kuwa watoto wao wamelogwa pindi wanapokosa huku wakiacha kufika hospital na badala yake kwenda kwa waganga wa jadi.
Katika hatua nyingine aliwataka viongozi na wananchi wa mkoa wa Iringa kuendelea kuyatunza majengo hayo ambayo yamejengwa kwa fedha za wahisani .
" kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kuhujumu miundo mbinu ya serikali kwa kuiba vifaa mbali mbali kwa madai kuwa ni mali ya serikali .....hili si jambo jema lazima wote tushirikiane katika vifaa hivyo ambavyo ni mali ya watanzania wote"
Mama Kikwete amesema kuwa kwa upande wake ataendelea kutoa ushirikiano kwa Hospital hiyo katika kutatua changamoto mbali mbali ikiwemo ya ushauri na kufikisha changamoto hizo sehemu husika.
Japo alisema kuwa suala la uhaba wa madaktari serikali ni suala ambalo tayari serikali imeanza kulifanyia kazi ni pamoja na kuendelea kuongeza madaktari katika kuwapa mafunzo madaktari wapya ambao wataweza kuongezwa katika Hospital hapa nchini.
Alisema kuwa maambukizi ya UKIMWI Iringa ni asilimia 9.1 ambapo ni sawa na watu 9 kati ya 100 mkoani Iringa wameathirika idadi ambayo ni kubwa kuliko ile ya taifa ya wastani wa watu 5 ambao wameathirika hivyo mkoa wa Iringa bado upo juu kwa maambukizi hayo.
" Watu wa Iringa ari zaidi nguvu zaidi mmeiwaka katika maambukizi ya UKIMWI hivyo nawaombeni sana watu wa Iringa kujilinda zaidi na kuepuka kusaliti ndoa zenu na wale ambao bado kuona ama kuolewa basi kujiheshimu zaidi"
Pia aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara na wale ambao watabainika wameathirika wasisite kutumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI na kuachana na tabia ya kuacha matumizi ya dawa hizo.
Huku wale ambao bado hawajaambukizwa basi kutulia na kujilinda ili wasipate maambukizi hayo na kuwaomba wanawake wajawazito ambao watakubwa na maambukizi ya VVU basi kufika Hospital na kupima ili kuwezesha watoto kuzaliwa bila maambukizi.
Wakati huo huo mama Kikwete aliwataka wanaume ambao bado kupatiwa huduma ya Tohara kujitokeza kufanyiwa huduma hiyo ili kusaidia kupunguza maambukizi ya VVU.

No comments:
Post a Comment