Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamili alisema pamoja na kughushiwa kwa majina hayo, robo tatu ya wafugaji 400 wa jamii ya Kibarbeig katika eneo hilo, lenye hekari 4,030 hawapo kwenye orodha ya kupewa ardhi.
"Tunaomba Serikali isitishe kugawa ardhi hii, kwani baadhi ya viongozi wa vijiji wameghushi majina, kuna watu wamefariki na wengine ni watoto na ndugu za viongozi,"alisema Kamili.
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha
Mawakili Tanganyika, Fransis Stola, alitaka ugawaji wa shamba hilo
usitishwe kwa maelezo kuwa kuna mgogoro.
"Sheria za ardhi zipo wazi kwamba kunapokuwa na mgogoro kama huu, lazima suluhu ipatikane kwanza badala ya kuendelea kugawa ardhi,"alisema Stola.
Alikuwa akizungumzia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elasto Mbwilo, kuhusu kugawanywa shamba hilo.
Kwa zaidi ya miaka miwili sasa tangu serikali, kurejesha shamba hilo la Gawal kwa wananchi, kumeibuka mgogoro wa kugawanywa kutokana na wafugaji wa jamii ya Kibarbeig wanaoishi katika eneo hilo, kutaka kupewa kipaumbele lakini serikali inapinga.
Katika mgogoro huo, viongozi kadhaa wa Kijiji cha Mulbadau, katika Kata ya Basotu walijeruhiwa baada ya kutaka kugawa ardhi kwa nguvu.
Chanzo:mwananchi mtandaoni

No comments:
Post a Comment