Kwa mujibu wa walalamikaji, walinzi hao wanadaiwa kujiwekea utaratibu usiyo rasmi chini ya kampuni ya ulinzi wa eneo hilo iliyotajwa kwa jina la Omega Nitro Risk Solutions ya jijini Dar ambapo ‘vijana’ wake wanatuhumiwa kutoza watu faini ya shilingi elfu kumi kwa gari ambalo mhusika wake amepoteza kadi ya kuingia na kutoka.
Madai hayo yalikwenda mbele zaidi ikielezwa kuwa kumekuwa hakuna utaratibu mahususi kwenye ishu hiyo kwani baadhi ya walinzi kila mmoja hujiamulia kuchukua fedha bila mhusika kupewa risiti ya malipo.
“Kuna tatizo kwenye safu ya ulinzi, huwa tunatozwa faini shilingi elfu kumi ukipoteza kadi,” alisema mmoja wa walalamikaji hao.
Baada ya malalamiko kutua kwenye kitengo chetu cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM), kazi ilianza ambapo kikosi kazi kilifanya doria kwa siku kadhaa na kufanikiwa kunasa laivu hatua kwa hatua, tukio la walinzi hao wakilamba ‘kitu kidogo’.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika geti la Mlimani City la upande wa Barabara ya Sam Nujoma ambapo walinzi hao walizuia gari la jamaa aliyekuwa amepoteza kadi na kuchukua rushwa.
Katika hali ya kushangaza au njaa, tofauti na kiasi cha shilingi elfu kumi kilichotajwa awali, walinzi hao walikubali kumpunguzia jamaa huyo hadi elfu tano bila kujua kwamba walikuwa wakirekodiwa hatua kwa hatua.
Baada ya kujikusanyia ushahidi wa kutosha, OFM ilizungumza na bosi wao ambaye ni Senior Inspector wa Omega Nitro Risk Solutions, Leo John Masuka juu ya vitendo hivyo ambapo mbali na kuonesha kushangazwa na habari hizo, pia alianika kila kitu jinsi wanavyofanya kazi.
“Nashangaa kama kuna tatizo kama hilo kwani tumesitisha kuwatoza faini wanaopoteza kadi, nitafanya uchunguzi ili kuwabaini watu hao ambao wanaharibu sura ya kampuni.
Katika hali hiyo kwa kipindi hiki cha tishio la ugaidi ni rahisi kwa magaidi kutoa rushwa kisha kuingia na kufanya utekaji kama walivyofanya nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment