Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewataka Watanzania kuachana na hulka ya kukejeli jitihada za maendeleo
na kujenga fitina kuhusu miradi ya maendeleo.
Amesema
kuwa baadhi ya Watanzania, badala ya kuunga mkono jitihada za maendeleo,
wanapiga kasi mpya ya kurudi nyuma kwa kupinga na kukejeli miradi ya
maendeleo. (hd)
Rais
Kikwete alikuwa anazungumza leo, Alhamisi, Oktoba 3, 2013, Kisiwani
Mafia wakati alipoanza ziara ya siku tano kukagua shughuli za maendeleo
na kufungua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Pwani.
Akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Chuo cha Ufundi, Tereni, nje ya mji mkuu wa
Mafia wa Kilindoni, Rais Kikwete ameimwagia sifa Mfuko wa Maendeleo ya Mafia (MIDEF) ambao umefanikisha mambo makubwa ya maendeleo katika Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Chuo hicho ambacho kitagharimu kiasi cha sh. bilioni 5.33 na kuchukua wanafunzi 400 kitakapokamilika. Chuo hicho pia kitakuwa na sehemu ya Chuo cha Michezo – Sports Academy.
Mafia wa Kilindoni, Rais Kikwete ameimwagia sifa Mfuko wa Maendeleo ya Mafia (MIDEF) ambao umefanikisha mambo makubwa ya maendeleo katika Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Chuo hicho ambacho kitagharimu kiasi cha sh. bilioni 5.33 na kuchukua wanafunzi 400 kitakapokamilika. Chuo hicho pia kitakuwa na sehemu ya Chuo cha Michezo – Sports Academy.
Mbali na
ujenzi wa chuo hicho, MIDEF imejenga shule ya sekondari ya bweni,
imeunga mkono shule za sekondari za kata za Serikali kwa kuzipa kompyuta
na madawati, inatoa mikopo ya maendeleo kwa wananchi, imetoa zana za
kazi kwa taasisi za Serikali na imesimamia kupatikana kwa fedha za
kusambaza umeme katika vijiji vyote vya Mafia kupitia Mamlaka ya
Kusambaza Umeme Vijijini (REA).
Kwenye
mradi wa kusambaza umeme vijijini, kwa mfano, MIDEF imechangia kiasi cha
Sh. Milioni 500 katika mradi ambao utagharimu Sh. Bilioni tano.
Rais
Kikwete amewaambia wananchi wa Mafia: "Jitihada hizi za MIDEF lazima
ziungwe mkono. Sina maneno mazuri ya kuwaambieni kuwa kama hamtaunga
mkono jitihada hizo mtakuwa na matatizo, tena matatizo makubwa sana.
Mtakuwa mnafikia kwa kasi mpya ya kurudi nyuma."
Amesisitiza
Rais Kikwete: "Nasema hivyo kwa sababu sisi Watanzania kazi yetu
imekuwa ni kujenga fitina, kubeza na kukejeli jitihada za maendeleo.
Hiyo ndiyo hulka yetu kujenga fitina kuhusu miradi ya maendeleo."
"Tunashangaza
sana. Mtu anayekuhubiria upate maendeleo unamwona mtu mbaya, lakini mtu
anayekuhubiria usipate maendeleo unamuona mtu mzuri na mwema. Tabia hii
ndiyo naiita ya kupiga kasi mpya ya kurudi nyuma," amesema Rais
Kikwete.
Katika
ujenzi wa Chuo hicho cha Ufundi, Serikali imechangia kwa kutoa ardhi ya
kujenga chuo hicho katika eneo la Tereni na kukamilika kwa Chuo hicho
kuitaiwezesha Tanzania kuongeza idadi ya vyuo vya ufundi nchini. Kwa
sasa kuna vyuo vya ufundi 742 vyenye wanafunzi 145,510, kati ya hivyo 17
vikiwa vya Serikali, na vilivyobakia vikiwa vya watu na taasisi
binafsi.
Rais
Kikwete ambaye ameshinda siku nzima katika Wilaya hiyo ya Mafia amerejea
Dar Es Salaam jioni ya leo na kesho atafanya ziara ya Wilaya ya
Mkuranga.
No comments:
Post a Comment