Mabingwa hao mara nne Afrika tayario walikuwa mbele kwa mabao mawili hadi mapumziko, yaliyofungwa na mshambuliaji Mtanzania, Thomas Ulimwengu dakika ya 21 na kiungo wa Ghana, Daniel Nii Adjei dakika ya 33.
Dakika tano baada ya kuanza kipindi cha pili, Gladson Awako wa Ghana pia alifunga la tatu kabla ya ndugu yake Richard Kissi Boateng kufunga la nne dakika ya 66.
Adjei akafunga bao lake la pili katika mchezo huo dakika ya 68 kabla ya Herve Ndonga kufunga la sita dakika tatu baadaye na Mtanzania mwingine, Mbwana Samatta akafunga la saba dakika ya mwisho.
Ushindi huo mnono unakuja siku chache kabla ya kucheza Nusu Fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stade Malien ya Mali wiki ijayo, baada ya awali kushinda ugenini 2-1 katika mchezo wa kwanza. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment