Mwenyekiti
wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA),Juma Pinto
akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii nje ya Ukumbi wa Mikutano
wa Water Front,kunakofanyika Uchaguzi wa Rais na viongozi mbali mbali wa
Shirikisho la Soka nchini (TFF) ambapo hadi sasa hakuna Mwandishi
yeyote alieruhusiwa kuingia kwenye Ukumbi huo kwa madai kwamba Waandishi
hawausiki na Uchaguzi huo,kwani waandishi jukumu lao ni kusubiria
kupewa matokeo tu ya uchaguzi huo,kauli iliyotolea na Mwenyekiti wa
Kamati ya Uchaguzi,Ndg. Hamidu Mbwezeleni.Jambo hilo liezua tafrani
kidogo kwenye Eneo hilo hasa pale Watu wa Usalama (Polisi) walipowataka
Waandishi kuondoka kwenye Eneo hilo la Uchaguzi.Mwenyekiti wa TASWA,Juma
Pinto amewataka Waandishi wa Habari kuachana na Uchaguzi huo na
kutoripoti chochote,kwani kilichoonyeshwa ni dharau kubwa kwa waandishi
wa Habari na watanzania wote nchini wanaopenda Michezo.CHANZO MICHUZI JR BLOG
Play Global yachochea Mapinduzi ya Baseball nchini Tanzania
-
*Na Mwandishi Wetu*
*DAR ES SALAAM – Juhudi za kuukuza mchezo wa baseball nchini Tanzania
zimepata msukumo mpya baada ya programu ya mafunzo iliyoandaliwa...
1 hour ago


No comments:
Post a Comment