Wakuu wa
nchi za Kenya,Uganda na Rwanda baadaye leo wanatarajia kusaini
makubaliano ya kuanzisha kituo kimoja cha kukusanya ushuru
kinachotarajiwa kurahisisha uchukuzi wa bidhaa kutoka Mombasa Kenya --
Uganda hadi Rwanda.
Kuundwa kwa Kituo hicho pia kunatazamiwa kurahisisha shughuli nzima za uchukuzi katika maeneo hayo ya Afrika Mashariki.
Taifa la Sudan Kusini pia linataraji kuidhinishwa kama mshirika katika kikao cha wakuu wa mataifa hayo.
Mkutano huu unalenga kuimarisha maendeleo ya kikanda kupitia kwa miundo msingi bora , uchumi na biashara.
Shughuli
hii inakuja baada ya mkutano uliofanyika mjini Kampala Uganda, mnamo
mwezi Juni na mwengine uliofanyika mjini Mombasa mnamo mwezi Agosti
ambako viongozi walipendekeza kupanuliwa kwa bandari ya Mombasa ili
kuwezesha uharaka wa bidhaa kupitishiwa bandarini humo katika kuhudumia
kanda nzima
No comments:
Post a Comment