MWANAMUZIKI
mkongwe wa Hip hop na Bongo Fleva kutoka mkoani Morogoro, ambaye pia ni
mfalme wa Rymes, Selemani Msindi 'Afande Sele' muda mfupi uliopita
amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya
kukabidhiwa kadi ya chama hicho na Powell Mfinanga wakati wa mkutano
mkubwa uliofanyika katika kata ya Mafiga na Misufini mkoani Morogoro!
Mwanamuziki
huyo toka zamani alikuwa na nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la
Morogoro kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 yawezekana ndiyo kaanza
safari rasmi leo.



No comments:
Post a Comment