IKIWA zimepita
wiki takribani mbili baada ya mwanaume mmoja kuzikwa akiwa hai eneo la
kijiji cha Mshewe wilaya ya Mbeya Vijijini mkoan hapa, mwanaume mwingine
wa kijiji cha Shilanga wilayani humo, amenusurika kuzikwa akiwa hai
jana.
Taarifa kutoka eneo la
tukio, zimemtaja mzee aliyenusurika kuzikwa akiwa hai kuwa ni Pascal
Mwanjalanje, aliyetuhumiwa katika kifo cha binti mmoja kijijini hapo
aliyekufa katika mazingira yanayodhaniwa kuwa ni ya utata.
Wakizungumza na kalulunga
blog, baadhi ya wananchi wa kijiji cha Shilanga, wamesema kuwa, kuna
binti wa kijiji hicho alikwenda kufua mtoni na baada ya kumaliza
aliwaambia wenzake kuwa anataka kupumzika, kisha akajilaza kwenye majani
na kifo kikampata akiwa amejilaza.
Kutokana na tukio hilo,
vijana wakachimba kaburi na kugomea kuuzika mwili wa mwanamke huyo kwa
madai kuwa hakukuwa na mtu aliyekufa hivyo akatafutwa mzee Mwanjalanje
anayetuhumiwa kumloga ili azikwe, na baada ya jitihada za kumzika mzee
huyo kugonga mwamba walifukia kaburi.na Kalulunga blog
No comments:
Post a Comment