Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, November 1, 2013

AUWA MJUKUU WAKE KWA KUMPIGA NA FIMBO KICHWANI BAADA YA KUMTUHUMU KUMUIBIA DEBE MOJA LA MAHINDI‏

Na Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikila Zenobi  Lusale (65)  Mkazi wa Kijiji cha Sibwesa Tarafa ya Karema Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumuuwa mjukuu wake kwa kumpiga na fimbo kichwani baada ya kumtuhumu kumwibia debe moja la mahindi

Kwa mijibu wa Kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Joseph Shilinde  tukio hilo lilitokea hapo jana majira ya saa kumi na moja jioni katika kitongoji cha senta Magogo Kijiji cha Simbwesa  Tarafa ya Karema Wilayani hapa

Kaimu kamanda Joseph Shilinde alimtaja aliyeuwawa kwa kupigwa na fimbo kichwani na babu yake kuwa ni  Stansilaus Joseph (15) Mkazi wa kijij hicho

Siku hiyo ya tukio  mtuhumiwa Zenobi  alikwenda kwa jirani kunywa pombe ya kienyeji aina ya komoni   mida ya mchana na kisha aliporejea nyumbani kwake  aliko kuwa akiishi na mjuu kuu wake huyo  na ndipo alipo mwita  kwa lengo la maongezi

Marehemu aliitika wito huo wa Babu yake kwa kujua wanataka kufanya mazungumzo  kama ambavyo wamekuwa wakifanya yeye na Babu yake mara kwa mara

Kaimu Kamanda alieleza kuwa ndipo mtuhumiwa alipoanza kumshutumu  marehemu mjukuu wake kuwa kuna mahindi debe moja yameibiwa ndani na yeye marehemu ndiye aliyeiba  mahindi hayo

Marehemu baada ya kuambiwa tuhuma hizo alimkatalia katakata Babu yake kuwa yeye haja iba mahindi hayo  labda aliuza mwenyewe  na  amesahau kama alimuuzia mtu kwani yeye hana tabia ya wizi

Mtuhumiwa baada ya kujibiwa hivyo na marehemu  alianza kumshambulia kwa fimbo kichwani huku mjukuu wake huyo  akipiga mayowe na  ya kuomba msaada   na huku akimsihi babu yake asiendelee kumpiga  lakini hakufanya hivyo aliendelea kumpa kichapo tuu

Majirani walifika katika eneo hilo na kumkuta mtuhumiwa akiwa ameshika fimbo hiyo aliyotumia huku marehemu akiwa amegalagala chini na huku akiwa ameishafariki dunia kutokana na kipigo hicho  na majirani hao walimkamata mtuhumiwa na kumweka chini ya ulinzi

Polisi walifika kwenye eneo hilo  na kumkuta mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi wa wanakijiji hicho na ndipo walipomchukua hadi katika kituo cha polisi cha Mpanda Mjini

Shilinde alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospital ya Wilaya hii na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara uchunguzi wa tukio hili utakapo kuwa umekamilika

No comments:

Post a Comment