Freeman Mbowe
Mkurugenzi wa Oganizasheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kilichojiri kwenye mkutano wa Kamati Kuu (CC)unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Alisema suala hilo litajadiliwa kwenye kikao hicho na taarifa itatolewa na mwenyekiti, Freeman Mbowe, (pichani chini).
Kigaila aliongeza kuwa ajenda zilizojadiliwa ni hesabu zilizokaguliwa na zilizopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa, yatokayo na vikao viwili vya dharura vya CC, upangaji upya wa kurugenzi ya chama makao makuu na nguvu kazi ili kutekeleza majukumu vizuri.
Nyingine ni uundaji na ujenzi wa chama ngazi za chini ambazo ni msingi wa chama na kwamba kwa sasa wanajadili kanda ya ziwa mashariki yenye mikoa ya Mara, Shinyanga, na Simiyu yenye majimbo 19 na wapiga kura ,milioni 1.7
Alisema ajenda ya mwisho itahusu hali ya kisiasa ndani na mahusiano ya kimataifa.
Alisema suala la aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, halitajadiliwa kwa kuwa mamlaka ya nidhamu ya kanda yake na kama atapenda kukata rufaa ndipo lingeweza kujadiliwa na hadi sasa hajafanya hivyo.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment