skip to main |
skip to sidebar
Dawa za kulevya: Watanzania watatu wadaiwa kukamatwa India, mmoja afariki
|
picha na maktaba |
Kuna taarifa kuwa Watanzania wawili wamekamatwa na dawa za kulevya
nchini India na kwamba mmoja wao amefariki dunia. Taarifa zinadai kuwa
Watanzania hao, ambao walikuwa watatu, waliwasili katika uwanja wa
kimataifa wa ndege wa Chatrapati Shivaji juzi asubuhi na Ethiopian
Airlines Flight 610.
Baada ya kutua uwanjani hapo, maafisa kutoka uwanjani hapo waliwakamata
Watanzania wawili kati ya watatu kwa mahojiano zaidi baada ya kutonywa
(tip-off) kuwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya. Baada ya kuhojiwa kwa
muda wa masaa matano, Watanzania hao walikataa katakata kuwa walikuwa
"punda" wa dawa za kulevya.
Taarifa zinadai kuwa maafisa hao waliamua kuwapa Watanzania hao chakula
na maji kama trick ya kujua kama walikuwa wamebeba dawa za kulevya. Kwa
kawaida, mtu aliyemeza vidonge vya dawa za kulevya hali wa kunywa ili
kuepukana na kifo. Hivyo basi, kama mtuhumiwa akipewa chakula na kukataa
kula inaweza kuwa ni dalili kuwa amemeza vidonge vya dawa za kulevya.
|
picha na maktaba |
Hivyo basi, baada ya kupewa chakula na maji, Mtanzania mmoja alikataa
kula wala kunywa. Hata hivyo, Mtanzania wa pili alikubali kula chakula
alichopewa. Baada ya hapo, Watanzania wote watatu walipelekwa
mahakamani, lakini yule aliyekubali kula alikataa na kutaka kukukimbia.
Baada ya purukushani katika eneo la mahakama, yule aliyekubali kula
chakula alifariki baada ya kuzidiwa na vidonge vya cocaine kama 120
alivyokuwa amemeza.
Hali ya Mtanzania wa pili ilizidi kuwa mbaya na alipelekwa katika
hospitali ya JJ. Baada ya kufanyiwa X-ray na CT-scan alikutwa amebeba
vidonge vya cocaine kama 100 hivi. Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa
hosipitali hiyo, hali yake ni mbaya lakini hajapelekwa ICU.
Mtanzania wa tatu, ambaye ni mwanamke wa makamo, bado anahojiwa na
vyombo husika. Mwanamke huyo hakukutwa na dawa zozote lakini alikuwa
ameongozana na wanaume hao wawili. Upelelezi bado unaendelea kujua kama
alikuwa mmiliki wa hizo dawa za kulevya.
Habari kwa mujibu wa India Today, The Times of India, Daily News India
No comments:
Post a Comment