Alitakiwa kuondoa kifusi barabarani ili ofisa mmoja wa
masuala ya usalama apite, akashindwa kwa vile katapila liliharibika,
akaishia kuchapwa viboko hadharani
Njombe. Mtu anayedaiwa
kujihusisha na masuala ya ulinzi na usalama Wilaya ya Ludewa, anadaiwa
kumshambulia kwa kumchapa bakora mfanyakazi wa Kampuni ya Boimanda
Modern Construction Company Ltd (BMCC) Alphonce Lutengano (25)
inayofanya ukarabati wa kilomita 56.5 za Barabara ya
Njombe-Ludewa-Manda.
Tukio hilo la aina yake limetokea hivi karibuni
katika Kijiji cha Muholo, Kata ya Luana Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe
wakati mfanyakazi huyo akiwa kazini, baada ya ofisa huyo kukuta vifusi
vimemwagwa katikati ya barabara wakati akipita kwenda Kata ya Lugarawa
kwenye shughuli zake.
Apigwa akiwa kazini
Lutengano anadai kuwa akiwa kazini na mtumishi
mwenzake Mary Luca wakisubiri katapila lao lililokuwa linazibwa baada ya
gurudumu moja kupata hililafu ili kusambaza vifusi hivyo, ofisa huyo
alifika eneo hilo akiwa na mwenzake ndani ya gari akitumia gari aina
Nissan Hard Top, alianza kumhoji kwa nini wamemwaga kifusi katikati ya
barabara na kumtaka akitoe ili apitishe gari lake kwa madai kuwa
haliwezi kupita pembeni kama walivyomshauri.
“Aliponihoji nilimwambia tunasubiri katapila ili
tuweze kusambaza kifusi, kwani wakati huo lilikuwa linazibwa baada ya
gurudumu moja kuishiwa upepo. Nikamshauri apite pembeni, akakataa
akisema nisambaze kifusi haraka ili apite akidai kuwa gari lake haliwezi
kupita pembeni. Alisisitiza kuwa tufanye hivyo haraka vinginevyo
atanipa adhabu,” anasema na kuongeza.
“Nilidhani utani, ghafla kweli akachuma fimbo ya
mti na kuanza kunipiga huku mwenzake akishuhudia, baada ya kuona hivyo
mwenzangu alikimbia ndipo nikatoa taarifa kwa mkuu wangu wa kazi Ludewa
akaja na polisi wakamkuta”.
Baada ya polisi kujibiwa hivyo walimwacha kwa madai kuwa aende akaendelee na majukumu yake baada ya hapo aripoti kituoni.
Shuhuda anena
Shuhuda wa tukio hilo Mwalimu mstaafu Gerald
Meshack Hiluka mkazi wa Muhola akielezea mkasa huo anasema “Mimi niliona
mtu anachapwa wakati natoka kumwagilia bustani, sasa nikabaki nimeduwaa
kwa mshangao, na sikujua anayemchapa kijana huyu ni nani kwa kuwa
nilikuwa napita, hivyo nikabaki naangalia tu”.
Kwa upande wake, Mary Luca anasema baada ya kuona
hivyo aliamua kukimbia ili kujinusuru na kipigo ambacho kingeweza hata
yeye kumpata.
Fundi Sanifu wa BMCC , Taji Omary alikiri kupokea
taarifa ya kupigwa mfanyakazi na kutoa taarifa Kituo cha Polisi Ludewa
wakaongozana kwenda eneo la tukio lakini walipofika licha ya polisi
kumkuta mtuhumiwa walimwacha aendelee na safari yake kana kwamba tukio
alilotenda ni jema kwa jamii.
chanzo;mwananchi.
chanzo;mwananchi.
No comments:
Post a Comment