Hitmaker wa Kimugina Linex Sunday amesema amekabidhiwa mtoto wake
Richard Sunday kutoka kwa mpenzi wake ambaye alimficha
kutokana usalama wa Linex wakati wa mahusiano yao
Akizungumza na Bongo5 leo, Linex alisema alikuwa hatambui kama ana
mtoto mwenye umri wa miaka nane kwakuwa alifichwa na mpenzi wake
kutokana na
mambo ya kifamilia kati ya wapenzi hao wawili.
Kweli nimefurahi sana kupata kitu ambacho haukukitegema.
Kwa sasa nimetoka kumchukua katika shule ambayo alikuwa
anasoma nataka kumhamisha, amesema Linex
Unajua mambo ya wanaume jinsi tulivyo,mimi nimeshindwa kuruka
kwasababu kitu alicho kifanya ni cha kijasiri sana
Hata hivyo Linex amesema hataki kusema nini kilitokea
kati yake na mzazi mwenzake kwakuwa anaandaa
documentary ya tukio hilo itakayokuwa
na mambo mengi excusive kuhusu yeye na mahusiano
yake pamoja na mtoto itayotoka wiki ijayo na
kuisambaza kwenye TV mbalimbali
No comments:
Post a Comment