Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 13, 2013

Imani za kishirikina, vurugu zinavyouchafua Mkoa wa Mbeya


 
Matukio ya masoko kuungua moto kama soko hili mkoani Mbeya yamekuwa ya kawaida. Kwa mujibu wa uchunguzi wa Taasisi ya Muungano wa Jamii, matukio ya moto yanatokana na imani za kishirikina.Picha  ya Maktaba.
Imani hizo zimesababisha watu watano kuzikwa wakiwa hai, masoko kuungua, watu kuchunwa ngozi na kujeruhiwa kwa nondo.
Siri ya migogoro na matatizo ya vurugu mkoani Mbeya yakiwamo ya kuungua kwa masoko imefichuka, baada ya machifu kupitia Taasisi ya Muungano wa Jamii Tanzania (Mujata) kugundua kuwa ni ushirikina uliokithiri wa wafanyabiashara. Machifu wanasema vitendo hivyo kwa kiasi kikubwa vinachangia kuvuruga kasi ya maendeleo ya mkoa huo.
Kwa mujibu wa Mujata, hata viongozi nao hasa wale wa kisiasa wanachangia kuwepo kwa hali tete mkoani humo, kwa kushindwa kuwapa taarifa wananchi, huku wengine wakijiingiza katika ufisadi kupitia wananchi.
Masoko kuungua mara kwa mara
Mwenyekiti wa Mujata nchini, Chifu Shayo Masoko anasema chanzo cha masoko kuungua mkoani humo, ni kuwepo kwa imani za kishirikina miongoni mwa wafanyabiashara wanaolezwa na waganga kuwa wakichoma moto mali zao na za wenzao watapata utajiri zaidi.
Taarifa zilizopo tayari masoko manne mkoani humo yameshaungua moto, japo vyanzo vyake havikuwa vikihusishwa na imani za kishirikina. Kwa mfano, mwaka 2006 Soko Kuu la Mkoa wa Mbeya  la Mwanjelwa liliteketea kwa moto katika mazingira ya kutatanisha na kuwafanya wafanyabiashara karibu 800 kuhamishiwa kwenye eneo la Sido ambapo walijenga vibanda vya soko jipya, lakini likaungua tena baada ya mwaka mmoja.
Mwaka 2009 Soko la Tunduma liliko mpakani mwa Tanzania na Zambia liliungua na baadaye mwaka 2010 soko kongwe la  Uhindini jijini hapa liliteketea kwa moto  katika mazingira ya kutatanisha.
Hata hivyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja anasema Serikali inaamini kwamba masoko ya Mwanjelwa na Uhindini yaliungua kutokana na  hitilafu ya umeme, wakati lile la Sido liliungua kwa moto wa mama lishe.
Kwa upande wa Mujata,  Chifu Masoko anasema kutokana na kukithiri kwa  matukio hayo, viongozi wa taasisi yake walikutana na kupokea taarifa za  walinzi wa kijadi,   waliotoa taarifa kwamba siri ya kuungua kwa masoko hayo ni ushirikina uliokithiri.
Walisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara waliahidiwa kupata mtaji mkubwa kama wangeunguza moto bidhaa zao na za wafanyabiashara wengine.
’Katika uchunguzi wa kimila tulibaini kwamba mpango huo ulitaka kufika kwenye masoko ya Mbalizi na Wilaya ya Momba, jambo ambalo tulilazimika kufanya mikutano ya hadhara kukemea waziwazi tabia hiyo ya ushirikina’’ anasema.chanzo mwanainchi

No comments:

Post a Comment