.Madaktari bingwa Nchini Mexico wasema anaweza kutibiwa na Viagra
.Upasuaji wake waweza usiwe salama
Na Damas Makangale, Moblog kwa Msaada wa Mtandao
Mvulana
mdogo wa umri wa miaka (15) ana uvimbe mkubwa Shingoni unaomsababishia
kushidwa kupumua vizuri lakini madaktari bingwa wanasema anaweza
kutibiwa kwa kutumia Viagra.
Jose
Serrano wa Ciudda d Juarez, Mexico alikuwa akiona ukuaji wa uvimbe
shingoni ukikuwa kila siku na kutishia maisha yake na ushauri wa
madaktari unasema oparesheni ya kawaida inaweza kuleta madhara katika
sehemu muhimu ya kiungo chake (shingo).
Taarifa
zinasema kuwa ugonjwa huo unajulikana kama (Lymphangioma) ni uvimbe
ambao dawa yake ni Viagra ambayo ni maarufu kwa kusaidia kuongeza nguvu
za kiume lakini kwa upande mwingine ni dawa ya uvimbe.
Jose mwenyewe anasema kuwa ana matumaini kuwa siku moja ataweza kuishi maisha ya kawaida kama vijana wengine.
“Kama
madaktari wanaweza kunitibu mimi itakuwa ni siku ya furaha, Napenda
kuwa na afya na ningependa kuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote
nikitaka,” amesema
‘
Lakini wakati mwingine anapata huzuni kwa sababu yeye ni tofauti na
watoto wengine. Hadi sasa hatujapata fedha ya kumtibu,” amesema baba
yake Jose Ramirez.
Jose Serrano akiwa na wazazi wake.CHANZO MO BLOG
No comments:
Post a Comment