.Arusha Mwasisi
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei amesema kuwa
chama hicho kitaendelea kuwafukuza wote wanaokihujumu huku akieleza
kwamba, anaunga mkono kuvuliwa uongozi kwa Zitto Kabwe na Dk Kitila
Mkumbo.Akizungumza
katika mahojiano nyumbani kwake jana, Mtei aliyewahi kuwa Gavana wa
Benki Kuu (BOT) na Waziri wa Fedha katika utawala wa awamu ya kwanza wa
Mwalimu Julius Nyerere, aliweka wazi kuwa daima ataunga mkono dhamira ya
kukisimamia chama hicho aliyoitaja kuwa ni safi. “Naunga
mkono uamuzi wote wa Kamati Kuu, kuwasimamisha na kuwavua uongozi Naibu
Katibu Mkuu wetu Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo. Na kwa sababu Chadema
inataka kusonga mbele, lazima iwafukuze mafisadi na wezi
wanaoshirikiana kukihujumu chama,” alisema Mtei.Bila
kufafanua zaidi au kutaja majina, mwenyekiti huyo wa kwanza wa Chadema
alisema: “Hatuwezi kuendesha chama wakati viongozi wengine wanapokea pesa na
kuzihifadhi kwenye akaunti za siri.” Alisisitiza kwamba kwa nafasi yake
akiwa mwasisi wa Chadema ni lazima ahakikishe anaunga mkono dhamira
safi ya kukisimamia chama.
Kuhusu Arfi kujiuzulu
Akizungumzia hatua ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Saidi Arfi kujiuzulu, Mtei alisema kuwa inafaa kiongozi huyo ajitazame upya na kujisahihisha badala ya kuwa mlalamikaji kila siku.
“Aache
kulalamika kwa sababu, wakati alipochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti mimi
nilisimamia uchaguzi. Kama alikuwa na ndoto kwamba siku moja atakuwa
mwenyekiti wa Chadema taifa alipaswa kujichunguza kwanza,” alisema.
Mtei
aliongeza kuwa iwapo kuna watu wanadhani Chadema itakufa hiyo ni dhana
potovu, lakini kwa sasa chama hicho kimejipanga kuchukua dola na tayari
wamejiimarisha kimkakati.
“Katika
suala la kushughulikia watu wanaokihujumu chama hakuna ‘compromise’
(mjadala),” alihitimisha Mtei. Juzi Chadema ilitangza uamuzi wa Kamati
Kuu yake kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dk Kitila, huku Arfi akitangaza
kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara.
Mtei
amewahi kumkemea na kumwonya Zitto katika mambo mbalimbali aliyofanya
ndani ya Chadema, moja ikiwa Oktoba mwaka jana ambapo mbunge huyo wa
Kigoma Kaskazini, alipotangaza kuwania urais mwaka 2015.
Alisema
kuwa hatua hiyo itasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama, huku
akiongeza kwamba amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua
yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana-Chadema na siyo kuwagawa au
kuwavuruga.
“Hakuna
shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza
sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na
siyo kukigawa wala kukivuruga,” alisema Mtei.
Mtei
alisema hatua ya mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala
yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015, imekuja mapema mno na kuonya
kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema, akiweka wazi kuwa wakati ukifika
chama hicho kitafanya uchaguzi sahihi.
“Siyo
vibaya kwa Zitto kuonyesha hisia zake, lakini ndani ya Chadema kwa sasa,
kuna watu mbalimbali wanaopenda kuwania urais, lakini hawajatangaza. Dk
Slaa (Willbrod) anataka,Freeman (Mbowe) anataka, Zitto anataka, hata mimi huenda nikataka kugombea. Hapa hakuna upendeleo, sifa ndizo zitakazoamua,” alisema.
Hata hivyo, Zitto alipinga kauli hiyo akisema: “Demokrasia haileti mizozo kwenye vyama vya siasa hata siku moja, bali humaliza mizozo. Udikteta, kuminya fikra huru na mawazo huru, ndivyo huleta mizozo kwenye vyama vya siasa.”
Alisema
ni muhimu wazee wakawaacha vijana wawe huru kusema wanachofikiri, kwa
kuwa uhuru wa fikra na mawazo ni moja ya haki za msingi na moja ya nguzo
za demokrasia.
“Ninarudia, nitaomba kupeperusha bendera ya
chama changu kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2015. Naamini kwamba
ninaweza kuwezesha chama chetu kushinda na kuongoza dola na Chadema
kutoa rais wakati baadhi ya waasisi wetu wakiwa hai na kuona vijana wao
tunavyobadili maisha ya Watanzania na kutimiza ndoto zao,” alisema
Zitto.
Alisema
ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kutosha kuwa Amiri Jeshi Mkuu na
kuunganisha Watanzania kuwa wamoja bila kujali rika, dini wala makabila
yao... “Nimejiandaa kisaikolojia kukabili changamoto za ufukara wa nchi
yetu.”
No comments:
Post a Comment