SAFARI YA KUELEKEA DSM YAANZA
§ MNAMO TAREHE
11.11.2013 MAJIRA YA SAA 14:10HRS HUKO KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA
MAITI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA JIJI NA MKOA WA MBEYA. JESHI LA
POLISI LILIWAKABIDHI MWILI WA MAREHEMU KASSIM SAIDI MBOYA NDUGU ZAKE
WAWILI AMBAO NI BABA WA MAREHEMU AITWAE SAID ATHUMANI MBOYA, MIAKA 60,
MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA – MCHANGANI – DSM NA MDOGO WAKE
NA MAREHEMU AITWAE HASSAN SAID MBOYA, MIAKA 28, MPOGORO, TINGO KAMPUNI
YA MOHAMED ENTERPRISES DSM, MKAZI WA MWANANYAMALA MCHANGANI –DSM.
§ BAADA
YA UTAMBUZI NDUGU HAO WA MAREHEMU WAMEMUELEZEA MAREHEMU NDUGU YAO
KUWA ALIKUWA ANAITWA KASSIM SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MPOGORO, MKULIMA,
MKAZI WA MWANANYAMALA-MCHANGANI –DSM.
§ AWALI
MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI
YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA.KASSIM SAIDI MBOYA, ALIFARIKI DUNIA
AKIWA KATIKA TARATIBU ZA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.
§ MAREHEMU
ALIKUWA ANASAFIRI KUTOKA DSM KUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI AKIWA
KATIKAM BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.319 BLZ AINA YA NISSAN
AKIWA NA HATI YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 PIA AKIWA NA BEGI DOGO
LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS, T-SHIRT MOJA NYEUSI, RABA JOZI MOJA
RANGI NYEKUNDU, MKATE MMOJA, MKOBA MDOGO WA KIUNONI, VACCINATION CARD
MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RAND MBILI SARAFU ZA AFRIKA YA
KUSINI NA MIFUKO SITA [06] YA RAMBO RANGI NYEUSI.
§ BASI
HILO BAADA YA KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE
GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU ZA KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI
MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA GARI HUKU HALI YAKE YA KIAFYA
IKIZIDI KUDHOOFIKA.
§ WAHUSIKA
WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA
NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO
KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA.
§ MWILI
WA MAREHEMU ULISAFIRISHWA HADI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA
UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA
KULEVYA ZIKIWA TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI YA PIPI HIZO IKIWA
IMEPASUKA, PIPI HIZO ZINA UZITO WA KILO 1 NA GRAM 140.TARATIBU
ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA
UCHUNGUZI WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA AINA YA MADAWA HAYO.
§ KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA
BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA, NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI PIA INAPUNGUZA NGUVU KAZI YA TAIFA.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Picha na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment