BONDA Manny Pacquiao amerejesha heshima baada ya kumpiga kwa pointi Brandon Rios mjini Macau asubuhi ya leo.
Mfilipino huyo alirejea ulingoni baada ya mwaka mmoja tangu apigwe kwa Knockout na Juan Manuel Marquez.
Na
alishinda kila raundi hivyo kuweka hai matumaini ya kupigana katika
pambano la dola za Kimarekani 300 dhidi ya Floyd Mayweather Jnr.
Alipata pointi 10 dhidi ya tisa kila Raundi katika Raundi 10 na mwisho wa siku akakusanya pointi 120 kwa 109. Chanzo: sportmail
No comments:
Post a Comment