Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba
akitoa ufafanuzi jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
jijini Dar es Salaam, juu ya kupungua kwa mgao wa umeme kutokana na
kufanikisha ukarabati wa visima vya gesi kwa zaidi ya asilimia themanini
na tano , kulia ni Meneja Uhusiano wa shirika hilo bi. Badra Masoud.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba (hayupo
pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akielezea juu ya
kupungua kwa mgao wa umeme kutokana na kufanikisha ukarabati wa visima
vya gesi kwa zaidi ya asilimia themanini na tano.(Picha zote na Eliphace
Marwa)
Na Hassan Silayo
Kampuni
ya Pan African Energy inayoendelea na Ukarabati wa visima vya gesi
imefanikiwa kukamilisha takriban asilimia 85 ya matengenezo katika
visima vya gesi vya songosongo.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO)
Mhandisi Felchesmi Mramba wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari leo
jijini Dar es salaam.
Mhandisi
Mramba alisema kuwa matengenezo hayo ambayo yanategemewa kukamilika
November 26 mwaka huu yameonesha mafanikio ikiwa ni pamoja na kuwa na
kasi ya kuridhisha kuliko ilivyotegemewa kwa kipindi cha mda mfupi tangu
matengenezo hayo yaanze.
“kwa
kweli napenda kuwaambia watanzania kuwa wenzetu wa Pan African
wanaoendelea na ukarabati katika visima vya songosongo wamekuwa na kasi
ya kuridhisha ambapo mpaka sasa wamekamilisha kiasi asilimia 85 ya
matengenezo na tunatarajia mapaka kufikia leo jioni tutaweza kuleta
asilimia 80 ya gesi na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la umeme hasa
katika kipindi hiki cha ukarabati wa visima hivyo.
Aidha
Mhandisi Mramba alifafanua kuwa matengenezo hayo ambayo yalienda
sambamba na kuzima mitambo kwenye visima hivyo yanafanyika kila mwaka
ili kuboresha uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi.
Akijibu
swali la waandishi wa habari waliotaka kujua kuhusu vigezo va ugawaji
wa umeme hasa katika kipindi hiki cha matengenezo Mhandisi alisema kuwa
maeneo muhimu kama kwenye mahospitali na sehemu za usalama yanapewa
kipaumbele kutokana na umuhimu wake katika jamii.
No comments:
Post a Comment