Mkuu wa
mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma akifungua mkutano wa siku ya ya
wadau mfuko wa bima ya afya mkoa wa Iringa kutoka kushoto ni kaimu
mkurugenzi wa NHIF Khamis Mdee,mwenyekiti wa bodi ya NHIF balozi Ali
Mchumo na kulia ni kaimu ras Bw Mwasumile na mkuu wa wilaya ya Mufindi
Evarista Kalalu
viongozi mbali mbali na wadau wakiwa katika mkutano huo leo katika ukumbi wa St Dominic
Mkuu wa
mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma wa tatu kushoto waliokaa akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufungua
mkutano wa siku ya ya wadau mfuko wa bima ya afya mkoa wa Iringa kutoka
kushoto ni kaimu mkurugenzi wa NHIF Khamis Mdee,mwenyekiti wa bodi ya
NHIF balozi Ali Mchumo na kulia ni kaimu ras Bw Mwasumile na mkuu wa
wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu.
Viongozi
wa kitaifa na mkoa wa Iringa waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa mfuko wa bima ya afya mkoa wa Iringa leo
MKUU wa
mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma amezitaka Halmashauri za wilaya
katika mkoa wa Iringa ambazo hazijawasilisha madai ya tele kwa tele
yenye jumla ya shilingi milioni 87 kwa ajili ya mfuko wa bima ya afya
kuwasilisha mara moja.
Pamoja na kuzitaka halmashauri hizo
kuwasilisha fedha hizo pia mkuu huyo wa mkoa alitangaza kuwachukulia
hatua kali watoa huduma katika vituo vya afya ambao wanahujumu mfuko huo
wa bima ya afya kwa kughushi huduma za matibabu za mfuko huo na mingine
ya afya.Mkuu huyo wa mkoa alitoa agizo hilo leo wakati akifungua mkutano wa siku ya wadau wa mfuko wa bima ya afya mkoa wa Iringa ,uliofanyika katika ukumbi wa St Dominic mjini Iringa .
Alisema kuwa zipo changamoto ambazo serikali ya mkoa wa Iringa imepata kuziona ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ikiwemo changamoto ya uchakavu wa baadhi ya vituo vya serikali kama vile Zahanati ya Isele, Ilolompya,Mapogoro ,Kising'a na Mtandika pamoja na upungufu wa dawa hasa katika vituo vya serikali .
Dr Ishengoma alisema kuwa serikali imejipanga kufanyia kazi changamoto hizo japo alisema hali ya uandikishaji wanachama wapya wa mifuko hiyo katika mkoa bado si ya kuridhisha mbali ya kuwa mkoa wa Iringa unaongoza kwa kuandikisha wanachama wengi katika Tanzania kwa kuwa nafasi ya nne kutimiza lengo la kuandikisha kaya 12,244 hadi juni 30 mwaka huu ambayo ni sawa na asilimia 9.6 ya malengo ya kuandikisha kaya 127,561 ifikapo mwaka 2014/15 .
Pia aliwataka watoa huduma kuhakikisha wanawapa huduma wanachama wa NHIF na CHF sawa na wananchi wengine bila ya ubaguzi wowote kwa kuwa mojawapo ya malalamiko yanayotokana na wanachama wa mifuko hiyo ni pamoja na kubaguliwa katika huduma kwa kuonekana kama watu wanaotibiwa bure mtazamo ambao si sahihi kwa maana gharama za matibabu kwa wanachama hao tayari zimelipwa kupitia mifuko hiyo.
" Nawaagiza watoa huduma wote kuacha mara moja tabia hiyo isiyozingatia utu ....watakaobainika kuwasumbua wagonjwa ambao ni wanachama wa mifuko hiyo tutawachukulia hatua kali zaidi "alisema mkuu huyo wa mkoa
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa aliwataka wanachama wa mifuko hiyo ya NHIF na CHF kuendelea kutumia kadi zao halali na kuachana na mpango wa kuazimishana kadi za matibabu ama kufanya biashara kwa kutumia kadi hiyo kwa ajili ya kughushi huduma za matibabu .
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya NHIF balozi Ali Mchumo(pichani juu) alisema kuwa katika kuhamasisha wananchi wengi zaidi kuendelea kujiunga na mifuko hiyo unaanzishwa utaratibu wa kutoa tuzo ya bima ya afya kwa wote kwa wilaya ambazo zitafanya vema katika kuingiza idadi kubwa zaidi ya wanachama.
Alisema kuwa lengo la serikali ni kuona watanzania wote wanapata huduma bora ya afya kwa kujiunga na mifuko hiyo hivyo ili kutimiza lengo hilo ni lazima kila kiongozi na kila wilaya kufanya uhamasishaji ili kila mtanzania kujiunga na mifuko hiyo.
No comments:
Post a Comment