Mrembo wa Taifa Redds Miss Tanzania 2013
Happiness Watimanywa yuko Kampala Uganda kwa mwaliko rasmi kutoka kampuni ya
Arapapa Fashion House & Design ya nchini Uganda.
Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa atakuwepo
nchini Uganda kwa muda wa siku 5 hadi tarehe 9 Novemba 2013 anatarajiwa kurejea
nchini.
Akiwa nchini Uganda ataungana na warembo wengine kutoka nchi
za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Kenya, Rwanda, Burundi na wenyeji Uganda.
Pamoja na mambo mengine warembo hao watahusika pia katika
kazi za jamii na baadaye kupanda jukwaani pamoja katika onyesho la mavazi
lililoandaliwa na Kampuni hiyo.
Kampuni ya Arapapa imekuwa ikifuatilia kwa karibu mashindano
ya urembo ya Miss Tanzania tangu mrembo Happiness anyakue taji na
waliazimia kumualika mrembo huyo kutembelea Uganda, jambo ambalo wamelitimiza.
Redds Miss Tanzania 2013 ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa
kwanza wa Shahada ya Juu katika Chuo cha Strathclyde nchini
Scotland, ameamua kuahirisha masomo yake kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi hapo
atakapovua taji mwishoni mwa mwaka 2014.
Mrembo Happiness Watimanywa atawakilisha Tanzania katika
mashindano ya urembo ya dunia hapo mwakani.
No comments:
Post a Comment