Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, November 5, 2013

SIMBA SC YAMJAZA DOLA 10,000 BABU MFARANSA, ETI NYINGINE ITAMMALIZIA MWAKANI

me_n_liewig_66b45.jpg
Kocha Mfaransa wa Simba SC kulia, akiwa na Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY...
Na Mahmoud Zubeiry, Kariakoo
KOCHA aliyetupiwa virago mwishoni mwa msimu Simba SC, Mfaransa Patrick Liewig leo amelipwa dola za Kimarekani 10,000 kati ya dola 18,000 anazoidai klabu hiyo kutokana na kufanya kazi tangu Januari hadi Mei, mwaka huu.
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa S.S.C., Joseph Itang'are 'Kinesi' leo amemlipa kocha huyo dola 10, 000, Kariakoo, Dar es Salaama na kuahidi kumuongeza dola 3,000 kesho na kwamba dola 5,000 atamaliziwa Februari mwakani.
Liewig alitua nchini siku mbili kabla ya mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga ambayo iliingiza zaidi ya Sh. Milioni 500 na alifikia katika hoteli ya Sapphire Court, Kariakoo, Dar es Salaam.(P.T)


Juni 20, mwaka huu Simba SC ilimlipa Liewig dola 10,000 kati ya dola 26,000 alizokuwa anadai klabu hiyo baada ya kumvunjia Mkataba na kuahidi kumlipa kiasi kilichobaki mwezi uliopita.

Liewig alikuwa anadai malimbikizo ya mishahara ya miezi miwili, dola 12,000 na dola 12,000 za kuvunjiwa Mkataba wakati dola 2,000 ni za tiketi yake ya kurejea kwake.
Kocha huyo alivunjiwa Mkataba wakati amepwa likizo ya kwenda mapumzikoni kwao, baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na nafasi yake amepewa Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibadeni'.
Hata hivyo, baada ya kurejea nchini alifanya mazungumzo na uongozi wa Simba, hatimaye wakakubaliana kulipana kwa awamu.
Liewig alisani Mkataba wa mwaka mmoja na nusu Januari mwaka huu kuifundisha Simba SC akirithi mikoba ya Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick aliyetupiwa virago.
Katika kipindi chake cha kuwa na klabu hiyo kwa miezi mitano, Liewig aliiongoza Simba katika mechi 25 akiiwezesha kushinda tisa, sare nane na kufungwa saba.

No comments:

Post a Comment