WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA MOTO.
MNAMO TAREHE 09.11.2013 MAJIRA YA SAA 21:00HRS HUKO MLIMA RELI, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA UTENGULE –USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA, FROLA D/O KYENGE, MIAKA 33, KYUSA, MHUDUMU WA BAR ,MKAZI WA MLIMA RELI ALITOA TAARIFA YA KUUNGUA MOTO NYUMBA ANAYOISHI NA KUTEKETEZA MALI ZOTE ZILIZOKUWA NDANI YA NYUMBA HIYO. NYUMBA ILIKUWA NA VYUMBA VITANO WANAVYOISHI WAPANGAJI WATANO TOFAUTI, IMEJENGWA KWA MATOFALI YA KUCHOMA NA KUEZEKWA BATI MALI YA JOHN S/O PONDAMALI MKAZI WA DSM. CHANZO KINACHUNGUZWA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA NA HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA, UPELELEZI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.
WILAYA YA MBOZI – WIZI WA MIFUGO.
MNAMO
TAREHE 08.11.2013 MAJIRA YA SAA 23:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA BARA,
KATA YA BARA, TARAFA YA IGAMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. SIMITON
S/O KABURU, MIAKA 36, MNYIHA, MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA BARA
ALIGUNDUA KUIBWA KWA MIFUGO[NG’OMBE] WAKE KUMI NA TATU[13] WENYE THAMANI
YA TSHS 6,000,000/= NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MBINU NI KUVUNJA ZIZI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO
MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI PAMOJA NA NG’OMBE WALIOIBWA ATOE
TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE MARA
MOJA.
WILAYA YA CHUNYA – AJALI YA GARI KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 09.11.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
CHALANGWA, KATA YA CHALANGWA, TARAFA YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA
MKOA WA MBEYA. GARI T.672 ASF AINA YA TOYOTA PRADO MALI YA KAMPUNI YA
UJENZI YA CHINESE COMMUNICATION & CONSTRUCTION LTD LIKIENDESHWA
NA DEREVA AZIZ S/O ABDALAH, MIAKA 30, MUHA, FUNDI MAGARI WA KAMPUNI
HIYO, MKAZI WA CHALANGWA LILIPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA HUYO
PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment