“PRESS RELEASE” TAREHE 26.11. 2013.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA GARI KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 25.11.2013 MAJIRA YA SAA 12:45HRS HUKO MAENEO YA MADUGU, KATA YA
ISANGATI, TARAFA YA ISANGATI BARABARA YA MBALIZI/UMALILA WILAYA YA
MBEYA MKOA WA MBEYA, GARI T. 966 BKR AINA YA MITSUBISH CANTER
LIKIENDESHWA NA DEREVA LUTIMO S/O SIMFUKWE, MIAKA 39, MNYIHA, MKAZI WA
MBALIZI LILIACHA NJIA KISHA KUPINDUKA NA KUSABABAISHA KIFO KWA YOHANA
S/O SOLOMONI, MIAKA 28, MNYAKYUSA, FUNDI MAGARI MKAZI WA DDC MBALIZI NA
MAJERAHA KWA ABIRIA 11. MAJERUHI WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA
IFISI MBEYA KWA MATIBABU. CHANZO CHA AJALI NI UTELEZI. DEREVA AMEKAMATWA
NA GARI LIPO KITUONI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI KATIKA KIPINDI
HIKI CHA MVUA ILI KUEPUKA AJALI.
WILAYA YA MBEYA MJINI – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 26.11.2013 MAJIRA YA SAA 05:00HRS HUKO MTAA WA ILEMBO AIR PORT,
KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, PELIS D/O
FREDRICK, MIAKA 35, MKINGA, MFANYABIASHARA SPAIR ZA PIKIPIKI MBALIZI NA
MKAZI WA ILEMBO AIR PORT ALIUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU KINACHODHANIWA
KUWA KISU SEHEMU YA UBAVU WA KULIA. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVAMIA MHANGA
AKIWA NYUMBANI KWAKE. MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA UKIWA NA MAJERAHA
MANNE SEHEMU ZA UBAVU WAKE WA KULIA, HAKUNA KITU CHOCHOTE
KILICHOCHUKULIWA NYUMBANI KWA MAREHEMU. CHANZO KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA
MMOJA AMEKAMATWA KUTOKANA NA TUKIO HILI DANIEL S/O TWEVE, MIAKA 21,
MKINGA, MFANYAKAZI WA DUKA LA SPAIR LA MAREHEMU MBALIZI NA MKAZI WA
TUNDUMA ROAD. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA
MBEYA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU
WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment