Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, November 2, 2013

Vipande 700 vya meno ya Tembo vimekamatwa maeneo ya Mikocheni - DSM

 
 Zaidi ya vipande 700 vya meno ya Tembo ambavyo vinakadiriwa kuwa ni zaidi ya tembo 200 kama wangekuwa hai vimekamatwa katika maeneo ya mikocheni jijini Dar Es Salaam ikiwa ni katika makazi ya raia wenye asili ya China.
ITV ilifika katika eneo hilo na kufanikiwa kushuhidia shehena hiyo huku baadhi ya raia wa China wakiwa chini ya ulinzi wa polisi ambapo mmoja ya Wachina hao amesema hahusiki  na mzigo huo na amekuja  nchini kwa ajili ya mapumziko.
Akizungumza katika eneo la tukio waziri wa malisi na utalii mh balozi hamis kagasheki amesema mapambo bado ynaendelea japo  wapo watu hasa wabunge wanaobeza jitihadaza hizo.
Katika hatua nyingine baadhi ya wakazi wa maeeno ya Mikocheni mtaa wa faru wamesema wanachojua ni kuwa Wachina hao wanafanya biashara ya kuuza ndimu na vitunguu.

No comments:

Post a Comment