Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
MUDA
mfupi baada ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kumteua Bw. Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa
TFF, Uteuzi ambao ni kuanzia jana Novemba 2 mwaka huu, kaimu katibu mkuu
huyo amesema yeye bado ni Afisa habari na ana kaimu nafasi hiyo ya
mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za TFF.
Akizungumza
na mtandao huu mchana huu, Afisa habari na kaimu katibu mkuu huyo mpwa
wa TFF, Boniface Wambura, amekiri kukabiliwa na majukumu makubwa zaidi,
lakini amesema kwanini ameteuliwa katika nafasi hiyo, Rais Jamal
Malinzi ndiye anaweza kueleza ni taraibu gani zimetumika.
“Cha
msingi ni kwamba, nahitaji ushirkiano kutoka wa wadau wote wa soka ili
kufika mbali, hapa tulipofika si haba, lakini tunahitaji kufika mbali
zaidi”. Alisema Wambura.
Wambura
alisema kiukweli majukumu yameongezeka kutoka nafasi yake ya Afisa
habari ambayo anaikalia mpaka sasa na sasa kaimu katibu mkuu, ila
ameendelea kusisitiza kuwa ushirikiano wa viongozi wote na wadau itakuwa
njia sahihi kwake yeye kutekeleza majukumu yake.
Pia
amesema taarifa zinazotolewa na mitandao mbalimbali kuwa kuna baadhi ya
watu wameondolewa katika nyadhifa zao, Wambura amesema wao hawafanyi
kazi kwa uvumi, kama ingekuwa hivyo basi taarifa kutoka kwa Rais Malinzi
ingetolewa.
“Kwa
sasa yanayozungumzwa ni uvumi, hakuna taarifa yoyote kama kumekuwepo na
mabadiliko, lakini kama kuna watu watabadilishwa nafasi zao, basi
taarifa kwa Umma itatolewa”. Aliongeza Wambura.
Katika
taarifa iliyotolewa leo na TFF aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile
Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.
Kamati
ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama
shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika
utekelezaji wa majukumu yake.
No comments:
Post a Comment