SOKA ni pesa. Ndivyo ilivyo duniani kote kwa sasa ambapo mchezo huo umegeuka na kuwa biashara kubwa kwa klabu na wachezaji husika.
Klabu zinaingiza fedha nyingi kwa mikataba minono
ya udhamini na zawadi. Ndiyo maana nazo zimefungua neema kwa wachezaji
na sasa zinawalipa mishahara minono na posho za uhakika, achilia mbali
fedha za usajili inazowapatia.
Ndio maana wanasoka nao wamegeuka kuwa matajiri
wakubwa, kwa Afrika wachezaji kama Samuel Eto’o na Michael Essien (wote
Chelsea) na Yaya Toure wa Manchester City, ni miongoni mwa wanaotajwa
kulipwa fedha nyingi.
Makala hii inakuletea orodha ya wanasoka 10 raia wa Kenya wanaolipwa vizuri katika klabu zao.
1. Victor Wanyama (Southampton, England)
Ni kiungo mkabaji ambaye pia ni nahodha wa timu ya
taifa ya Kenya, Harambee Stars. Wanyama mwenye umri wa miaka 22,
anapokea mshahara unaokadiriwa kuwa Sh314.3 milioni kwa mwezi.
Kiwango hicho ni mbali ya marupurupu anayolipwa
kwa kushiriki mazoezi au kila timu yake inaposhinda mechi. Hata hivyo
anakabiliwa na kiwango kikubwa cha ushuru unaotozwa na serikali ya
Uingereza hasa kwa raia wa kigeni.
Kabla ya kutua Southampton, Wanyama alikuwa
Scotland katika klabu ya Celtic ambapo alikuwa akilipwa Sh 1.2 bilioni
kwa mwaka, ilikuwa ni hesabu ya mshahara pekee.
Mwanasoka huyu anasemekana kuwa amewekeza nchini kwake kwa kununua viwanja na masuala ya ujenzi.
2. MacDonald Mariga (Parma, Italia)
Mariga, 26, ni kaka wa Wanyama. Anashika nafasi ya pili akiondoka na Sh251.5 milioni kwa mwezi. Ni hesabu ya mshahara pekee.
Jambo la kuvutia kwake ni kwamba Mariga huishia
kubaki na fedha nyingi kuliko mdogo wake kutokana na ushuru mdogo
anaotozwa na Serikali ya Italia.CHANZO MWANASPOTI
No comments:
Post a Comment