skip to main |
skip to sidebar
WAZIRI NCHIMBI AFUNGA MAFUNZO YA KOZI YA KUZIMA MOTO WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM
Wahitimu wa Jeshi wa Zimamoto na
Uokoaji wa kozi ya kuzima moto wa ndege wakizima moto kwenye ndege
bandia kabla ya mafunzo yao kufungwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Maofisa na Askari 21 wa jeshi hilo walihitimu
mafunzo hayo na kukabidhiwa vyeti katika hafla iliyofanyika jijini Dar
es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk.
Emmanuel Nchimbi akizungumza na wahitimu na wageni waalikwa kabla ya
kufunga mafunzo ya kozi ya uzimaji moto wa ndege. Maofisa na Askari 21
walihitimu kozi hiyo na kutunukiwa vyeti katika sherehe fupi ya kufunga
mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CG), Pius Nyambacha. Kulia ni Meja
Generali Kapwani, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk.
Emmanuel Nchimbi akimkabidhi zawadi ya cheti mwanafunzi aliyefanya
vizuri katika masomo darasani, Mohammed Shomari (kulia). Akizungumza
baada ya kuwakabidhi vyeti wahitimu 21 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
waliomaliza mafunzo ya kozi ya kuzima moto wa ndege, Waziri Nchimbi
aliwataka wahitimu hao wawe wahadilifu katika kazi zao wakiiheshimu
kazi. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CG), Pius
Nyambacha. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kikosi cha gwaride la wahitimu kikitoa
heshima mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa sherehe yao ya
kumaliza mafunzo ya kozi ya kuzima moto wa ndege kwa maofisa na askari
21 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliohitimu kozi hiyo jijini Dar es
Salaam leo. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye
aliyafunga mafunzo ya kozi hiyo aliwataka wahitimu hao wawe wahadilifu
katika kazi zao wakiiheshimu kazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
nchini (CG), Pius Nyambacha, akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) kwa kukubali wito wao wa kuja
kuyafunga mafunzo ya Maofisa na Askari 21 wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji waliohitimu mafunzo ya kozi ya kuzima moto wa ndege. Waziri
Nchimbi katika hotuba yake aliwataka wahitimu hao wawe wahadilifu katika
kazi zao wakiiheshimu kazi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment