Mshambuliaji
wa Yanga, aliyeingia kuchukua nafasi ya Didier Kavumbagu, Jerry Tegete,
akimtoka beki wa JKT Ruvu, Nashon Naftal, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu
ya Tanzania bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeshinda mabao 4-0, mabao mawili
yakifungwa na Mrisho Ngasa, katika dakika za 4 na 23 kipindi cha
kwanza, bao la tatu limefungwa na Oscra Joshuo, katika dakika ya 50 na
bao la nne limefungwa na Jerry Tegete katika dakika ya 86.
Jerry
Tegete (kushoto) akishangilia bao lake kwa staili ya kunong'oneza, huku
akipongezwa na Simon Msuva (kulia) na Mrisho Ngasa.
Didier Kavumbagu, akimfinya beki wa JKT Ruvu Mussa Zubery, wakati wa mtanange huo.
Simon
Msuva (kulia) akiruka daruga la beki wa JKT Ruvu na kuambaa na mpira,
ambapo alifanikiwa kutoa pasi nzuri iliyomkuta Hamis Kiiza, aliyeshindwa
kupata bao la wazi.
Sehemu
ya Jukwaa la mashabiki wa Simba, likiwa tupu, haikuweza kufahamika
sababu za kutohudhuria kama ilivyokuwa katika mechi za siku za nyuma.
Mashabiki wa Yanga, ilikuwa ni shangwe......
Hamis Kiiza, akipiga mpira wa kichwa na kusababisha heka heka langoni mwa JKT Ruvu.
Mrisho Ngasa, akiwafinya mabeki wa JKT Ruvu.....
PICHA KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO
No comments:
Post a Comment