Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 27, 2013

Zaidi ya wapiganaji 900 wameuawa katika mapigano ya hivi karibuni baina ya serikali na waasi wa M23 nchini DRC


Jenerali Jean-Lucien Bahuma/mulopwemustafa.

Mapigano kati ya jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na waasi M23 yalisabaisha vifo vya zaidi ya wapiganaji 900 katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo kabla ya wapiganaji waasi kufurushwa, afisa mwandamizi wa jeshi amesema leo Jumatatu.

Jenerali Jean-Lucien Bahuma afisa mwandamizi wa jeshi katika mkoa wa Kivu Kaskazini ambako mapigano yalifanyika amesema kuwa kati ya mwezi Mei tarehe ishirini na Novemba 5, wanajeshi wa serikali wapatao 201 waliuawa na wengine 680 walijeruhiwa ambapo kwa upande wa waasi wa M23 wapiganaji 721 waliuawa na 543 walikamatwa ikiwa ni pamoja na 72 raia wa Rwanda na 28 raia wa Uganda.

Aidha Jenerali Bahuma ameongeza kuwa walinda amani watatu wa Umoja wa Mataifa UN pia waliuawa katika mapigano hayo.

Waasi wa M23, moja ya makundi mengi yanayomiliki silaha katika eneo lenye utajiri wa madini lakini maskini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, waliangamizwa na jeshi la taifa, kwa msaada wa kikosi maalumu cha askari 3,000 wa Umoja wa Mataifa kilichoingilia kijeshi nchini DRCongo.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukiituhumu Uganda na Rwanda kwa kuwafadhili waasi wa M23 tuhuma ambazo hata hivyo zimepingwa vikali na nchi hizo mbili.

Matumaini kwa ajili ya mpango ya kisiasa wa kukomesha mauaji ya karibuni na uasi wa umwagaji damu uliolikumba eneo la Mashariki ya Congo yalisitishwa mnamo Novemba 12, baada ya serikali ya Kinshasa na wapiganaji waasi kushindwa kutia saini mkataba wa amani uliotumainiwa sana.

No comments:

Post a Comment