Ajali hiyo inahusisha gari lenye namba za usajiri T 829 AHH iliyokuwa
ikielekea katika soko la wiki maarufu kama MNADA. Gari hilo aina ya lori
limepata ajali maeneo ya kijiji cha Ilolanguru mbele kidogo ya chuo cha kilimo cha Tumbi kuelekea Urambo kwenye muda wa saa 4 asubuhi.
Dk. Kitapondya Deus, Mganga mfawidhi hospitali ya Rufaa ya Kitete mkoani
Tabora, ameuambia mtandao huu kuwa wamepokea wahanga 28 wa ajali hiyo
na miili minne (4) ya marehemu ambao tayari wametambulika na ndugu zao.
Pia mganga amesema wagonjwa wengine watasafirishwa na kupelekwa
hospitali ya karibu ambayo ni Nkinga.
Miili minne ya waliofariki katika ajali ya lori la mnada ambayo tayari imetambuliwa na ndugu zao.
Miili minne ya marehemu waliokumbwa na ajali ya lori la mnada
Wananchi waliojitokeza kushuhudia wahanga wa ajali ikiwa pamoja nakuwatambua ndugu zao waliohusika katika ajali hiyo.
Dereva anayehusika na ajali hiyo amekwishatiwa mbaroni na jeshi la polisi.
Chanzo cha ajali hiyo inasemekana kuwa na ubovu wa gari hilo ambalo lilikuwa na tairi lililokwisha (kipara)
No comments:
Post a Comment