Abiria kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu
na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya
ndege waliyokuwa wakisafiria kupasuka matairi yote manne ya nyuma wakati
ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Arusha leo mchana.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua, ambapo Matairi yote manne ya nyuma yalipasuka na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria.
"Yaani Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.Mh Lowassa ni mbunge wa Monduli, jimbo ambalo anatoka Waziri Mkuu aliyekuwa kipenzi Cha mwalimu Nyerere na watanzania hayati Edward Moringe Sokione.Sokoine aliyefariki katika ajali ya gari mwaka 1994.
No comments:
Post a Comment