Mkurugenzi
wa Taasisi ya kupambana na Kudhibiti Tushwa TAKUKURU Dk Hosea
akizungumza maadhimisho ya umoja wa mataifa ya kupambana na rushwa. Picha ya pamoja. Washiriki wa maadhimisho hayo .
………………………………………………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
NCHI za Afrika zimetakiwa kujenga umoja na kupeana uzoefu katika vita
vya kupambana na rushwa huku nchi hizo zikitakiwa kujenga sera za uwazi kwenye sekta nzima ya rasilimali ili waweze kunufaika nazo ikiwa ni pamoja na kupaza sauti moja kuomba kurejeshwa kwa fedha zilizoko nje ya bara la Afrika.
NCHI za Afrika zimetakiwa kujenga umoja na kupeana uzoefu katika vita
vya kupambana na rushwa huku nchi hizo zikitakiwa kujenga sera za uwazi kwenye sekta nzima ya rasilimali ili waweze kunufaika nazo ikiwa ni pamoja na kupaza sauti moja kuomba kurejeshwa kwa fedha zilizoko nje ya bara la Afrika.
Hayo yalielezwa jana na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia
Utawala Bora Mh.George Mkuchika alipokuwa akifunga na kusherehekea maadhimisho ya siku ya umoja wa mataifa ya mapambano dhidi ya rushwa pia maadhimisho ya miaka kumi ya mkataba wa umoja wa Afrika yaliyofanyika jijini Arusha.
Utawala Bora Mh.George Mkuchika alipokuwa akifunga na kusherehekea maadhimisho ya siku ya umoja wa mataifa ya mapambano dhidi ya rushwa pia maadhimisho ya miaka kumi ya mkataba wa umoja wa Afrika yaliyofanyika jijini Arusha.
Alisema kuwa elimu ina nguvu katika kupambana na rushwa hivyo ili
kuhakikisha kuwa swala hilo linatokomezwa na nchi za Afrika zinapaswa
kutekeleza kwa vitendo mkataba wa umoja wa Afrika dhidi ya rushwa kwa
kila nchi kujiunga moja kwa moja kwa kutoa uzoefu juu ya mapambano
dhidi ya rushwa ambayo yameonekana kurudisha nyuma maendeleo ya bara
la Afrika.
Alieleza kuwa pamoja na chi za Ulaya kuwa mstari wa mbele katika
mapambano dhidi ya rushwa lakini nchi hizo zimekuwa zikikumbatia
wahamishaji wa fedha kutoka bara la Afrika na kukaa kimya kila
wanapotakiwa kurejesha fedha zilizopo kwenye mataifa hayo.
“Mnakumbuka kwa kipindi cha nyuma wapo baadhi ya viongozi waliokamatwa
kwa kulimbikiza fedha katika mabenki ya nchi za nje ya bara la Afrika
hadi sasa fedha hizo bado hazijarejeshwa na mataifa hayo na mataifa
hayo kushikwa na kigugumizi licha ya kuhubiri vita dhidi ya rushwa
hivyo ni vema mataifa yetu ya bara la Afrika yakaungana kupaza sauti
ili fedha hizo zirejeshwe ili zisaide maendeleo ya bara la
afrika”aliongeza Mkuchika.
Aidha alifafanua kuwa nchi 30 zimesaini mkataba wa umoja wa mataifa
wa mapambano dhidi ya rushwa kati ya nchi 44 zinazotakiwa kusaini
mkataba huo hivyo kuzitaka nchi zilizobaki kujiunga na umoja huo ili
kuliletea maendeleo bara la Afrika na kuwa na sauti moja ya mapambano
dhidi ya rushwa huku akizitaka nchi za bara la afrika kutambua kuwa
mapambano ya rushwa si ya mtu moja bali ya watu wote.
Nae Mkurugenzi wa takukuru nchini Dr. Edward Hosea alisema kuwa bara
la Afrika bado lina safari ndefu katika mapambano ya vita vya rushwa
kwani kati ya nchi za afrika 34 kati ya 44 ndizo amabazo zimesaini
mkataba wa mapambano ya rushwa huku akidai kuwa mikataba mingi
inaingia kwenye rasilimali za nchi za bara la Afrika haina uwazi na
sheria zinazotumika hazimnufaishi mwananchi wa kawaida dhidi ya
mapambano ya rushwa.
Aidha Hosea aliitaka serikali kuweka sera ya uwazi kwenye mikataba ya
wawekezaji wa rasilimali ya gesi ili iweze kuwanufaisha watanzania na
sheria zitakazotungwa iwe ya uwazi na yenye faida kwa watanzania huku
akizishawishi nchi ambazo hazijatakeleza mkataba wa umoja wa mataifa
zifanye hivyo mara moja kwani bara la Afrika ndilo linalohitaji
maendeleo makubwa hivyo bila kuungana hawataweza kufanikiwa.
No comments:
Post a Comment