Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, December 13, 2013

MHE. BALOZI TUVAKO MANONGI AMWOMBELEZA MANDELA


 
Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi ameungana na     Wawakilishi wa  Mataifa mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa, katika kusaini kitabu cha  Maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa  Kwanza wa Afrika ya Kusini Huru, Mzee  Nelson Mandela. 

Kitabu hicho kimefunguliwa katika  Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya  Afrika ya Kusini katika Umoja wa Mataifa.  Katika Salamu zake,  Balozi Tuvako Manongi ameandika "  kwa niaba ya  Uwakilishi wa Kudumu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, ninawasilisha salamu zetu za rambirambi kwa  serikali,  wananchi, familia na  wapendwa wa Marehemu Mhe. Mzee  Nelson Mandela.  
Tunaungana nanyi katika kuombeleza msiba wa kiongozi huyo ambaye alijitolea katika  kuikomboa Afrika ya  Kusini. Mchango wake katika  kuwaunganisha wana wa afrika ya kusini  licha ya tofauti zao za kikabila ni  jambo lililoihamasisha dunia yote. Sisi katika  Tanzania tunajivunia sana  kumfahamu Madiba".

No comments:

Post a Comment