UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
TANZANIA INFORMATION SERVICES
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
anapenda kutoa mwaliko kwa makundi mbalimbali kwa ajili ya kuwasilisha
orodha ya watu wasiopungua wanne na waziozidi tisa kwa ajili ya
kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa kifungu
kidogo cha (2A) cha kifungu cha 22 cha sheria ya Mabadiliko ya Katiba,
sura ya 83 kinachomtaka Rais kuwaalika kila kundi lililoainishwa chini
ya kifungu kidogo cha (1) (c) kutoka pande zote za Muungano kuwasilisha
kwake orodha ya majina yasiyopungua 4 na yasiozidi 9 kwa ajili ya
kuzingatiwa katika uteuzi.
Makundi hayo ni kama ifuatavyo:
- Taasisi zisizokuwa za Kiserikali
- Taasisi za kidini
- Vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu
- Taasisi za elimu ya juu
- Makundi yenye ulemavu
- Vyama vya wafanyakazi
- Vyama vinavyowakilisha wafugaji
- Vyama vya wakulima
- Vyama vinavyowakilisha wavuvi
- Makundi mengine yenye malengo yanayofanana
Katika
kuwasilisha majina hayo, makundi yaliyoalikwa yatalazimika kuonesha
umri, jinsia, uzoefu, sifa na sehemu ya makazi ya mtu aliyependekezwa
ikiwa ni pamoja na kuzingatia usawa wa kijinsia.
Mheshimiwa
Rais ameelekeza kuwa orodha ya majina yanayopendekezwa yawasilishwe kwa
maandishi ama kwa kupeleka kwa mkono au kutumia huduma ya posta kwa
anuani zifuatazo:
- Katibu Mkuu Kiongozi,
Ofisi ya Rais, Ikulu,
S.L.P. 9120,
DAR ES SALAAM
- Katibu Mkuu Kiongozi,
Ofisi ya Rais,
S.L.P. 4224,
ZANZIBAR
Mwisho wa kupokea orodha ya majina hayo nitarehe 02 Januari, 2014
No comments:
Post a Comment