Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, December 13, 2013

ORODHA YA WASANII WAKUBWA TZ WALIOFARIKI GHAFLA NA WAKIWA BADO VIJANA,MUNGU AWALAZE MAHALA PEMA PEPONI

1. Steven Kanumba
Kifo cha steven kanumba ni moja ya kifo ambacho kilishangaza watu wengi sana. akiwa na umri wa miaka 28 tu , Kanumba ndio alikua msanii wa Bongo movies maarufu kuliko wasanii wote. Ni dhahiri kwamba kuliziba pengo aliloliacha ni vigumu sana. Inasemekana msiba wa kanumba ulihudhuriwa na watu wapatao 20,000. Kanumba aliaga dunia baada baada ya majibizano baina yake na elizabeth michael “lulu” yaliyomsababisha yeye kuanguka chini na kuumia kichwani mnamo april 7 , 2012 kitu kilichopelekea kifo chake. Hatuwezi kuongelea zaidi kifo chake kwasababu swala hili lipo mahakamani. Msiba  wake ulihudhuriwa na mke wa rais mama salma kikwete,  makamu wa rais , Dk. Mohamed Gharib Bilal na waziri wa utamaduni na michezo emmanuel Nchimbi.
rip kanumba

2. Albert Magwea
Kama wewe sio mpenzi wa bongo movies sana basi inawezekana kifo cha ngwea ndio kikawa kimekuuma zaidi. jamaa ni moja ya vichwa vya mistari na mashairi vilivyokua vimebaki. ngwea alifariki akiwa na miaka 31 tu na muziki kwake ulikua bado haujafa.  Ngwea naye alifariki akiwa  chumbani huko afrika ya kusini ambapo asubuhi kulipokucha jamaa alikua amelala fofofo, rafiki zake wakajaribu kumwamsha na kumwagia maji bila mafaniko ndo ikabidi wamwahishe hospitali ya St. Hellen ya jijini Johanesburg ambapo  madaktari walijaribu kuokoa maisha yake bila mafanikio, ndipo madaktari wakatoa ripoti kuwa msanii huyo ameaga dunia.
rip-ngwair

3. Sharo Milionea
Jamaa alipoteza maisha majira ya saa mbili hivi usiku tarehe 26 , November mwaka 2012 huko songa-maguzoni wilaya ya muheza mkoani Tanga . Husein Ramadhan Mkieti ‘SHARO MILIONEA’  alikua ni mchekeshaji pia muimbaji na amefariki huku akiacha mikataba mbalimbali na kampuni kama airtel , azam.
sharo-milionea

4. Cool James ‘mtoto wa dandu’
James Dandu alijulikana sana kama mtoto wa dandu. ni msanii aliyepoteza maisha mwaka 2002 kwa ajali ya gari iliotokea jijini dar-es-salaam. mtoto wa dandu alifanya muziki wake Tanzania na Sweden huku akiacha watoto wawili. James dandu alitamba na nyimbo kama sina makosa na mpenzi aliyomshirikisha mary G. Chakushangaza ni jinsi mtoto wa dandu alivyongelea kifo kwenye nyimbo yake ya sina makosa.
mtoto-wa-dandu
5.  Vivian na Complex
ilikua majira ya saa 3 asubuhi mwaka 2005 ambapo tasnia ya muziki iliwapoteza nyota wawili wa muziki ambao walikua wapenzi. Saimon sayi ‘complex’ ambaye alikua ni producer na rapper na vivian Tilya ambaye alikua ni mwanamuziki na mtangazaji wa clouds fm kwa ajali ya gari huko Mbwewe. Walipata ajali hiyo wakitokea morogoro kuelekea Arusha kwenye anniversary ya miaka 25 ya wazazi wa vivian.
rip-vivian-complex
Mungu azilaze Roho zao mahali pema peponi. Amen.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MOTOMOTO,PIA BOFYA HAYO MATANGAZO CHINI NA JUU KUJIFUNZA MAMBO MENGII(USIPITWEEE)

No comments:

Post a Comment