PADRE wa
Kanisa Katoliki Singida mjini Deogratus Makuri amefikishwa mbele ya
mahakama ya mwanzo Utemini mjini hapa akituhumiwa kushindwa kutunza
mtoto wake wa kike.
Ilidaiwa
mahakani hapo, kuwa Padre Makuri alikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa
muda mrefu na Maria Boniphance (26) mkazi wa Mitunduruni mjini hapa na
mhudumu katika parokia ya Singida mjini.
Ilidaiwa
mbele ya hakimu wa mahakama hiyo,Ferdnand Njau kuwa katika muda huo wa
mahusiano ya kimapenzi ndipo mdaiwa Makuri alipompa ujauzito Maria.
Maria aliiambia mahakama hiyo kuwa mara tu alipopata ujauzito huo alilifikisha tukio hilo kwa wazazi wake.
Amesema
wazazi wake walimwendea na bila kuuma ulimi alikubali kumpa uja uzito
Maria na kuahidi kwa maandishi kuwa atamtunza mtoto wake (jina tunalo)
hadi hapo atakapokuwa na uwezo wa kujitegemea.
Maria
amesema Padre ambaye inadaiwa kwa sasa amesimamishwa wadhifa wake huo
kutokana na tuhuma hiyo, alitekeleza ahadi yake hiyo kwa miezi michache
na kisha kugoma kuendelea kutoa matunzo.
"Baada ya
hapo nilimfikisha mbele ya ofisi ya ustawi wa jamii ambapo katika hati
ya mkataba, aliahidi kuwa atakuwa anatoa kila mwezi shilingi 80,000/= na
endapo atashindwa kutekeleza ahadi hiyo,aliomba afikishwe mahakamani
mara moja",amesema.
Ilidaiwa
kuwa pamoja na ahadi hiyo nzito,Padre Makuri alianza kudai kwamba mtoto
huyo sio mtoto wake wa kuzaa na kisha kuacha kutoa matunzo kama
alivyoahidi.
Katika
hatua nyingine,Maria amesema walianza mapenzi siku Padre huyo kumpa kazi
ya kufanya usafi kwenye kabati la vitabu chumbani kwakewakati
akiendelea kufanya usafi alifungiwa kwa nje hadi hapo usiku aliporejea
Padre akiwa na chakula cha jioni cha mhudumu Maria.
Amesema
Padre alimwambia kwa vile umekuwa ni usiku alale humo ndani na Padre na
kitendo hicho ndicho kilichoanzisha safari ya mahusiano yao ya kimapenzi
na kupelekea wapate matunda ya kuwa na mtoto.
Habari
zaidi kutoka kwenye parokia hiyo zinadai kuwa Padre Makuri alikuwa
kwenye maandalizi ya kwenda kuongeza elimu nje ya nchi.CHANZO MOBLOG
No comments:
Post a Comment