Mkurugenzi
wa Purosangue Athletic Club, Bw. Nico Angelo Pannevis (kushoto)
akimweleza jambo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel alipomtembelea
ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumueleza mpango wa
Klabu yake kushirikiana na Tanzania Kuwaendeleza Wanariadha chipukizi
nchini.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mkurugenzi
wa Purosangue Athletic Club, Bw. Nico Angelo Pannevis (katikati)
alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kumueleza mpango wa Klabu yake kushirikiana na Tanzania Kuwaendeleza
Wanariadha chipukizi nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Michezo, Bw. Leonard Thadeo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel (kushoto) na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo,
Bw. Leonard Thadeo (kulia) wakionyeshwa tisheti yenye logo ya Klabu ya
Purosangue Athletic ya nchini Italia leo Jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Mkurugenzi wa Klabu hiyo, Bw. Nico Angelo Pannevis. Klabu
hiyo imeonyesha nia ya kuendeleza vipaji vya Wanariadha chipukizi nchini
kwa kujenga kituo kwa ajili ya mpango huo.
Picha na Concilia Niyibitanga,
………………………………………………………………
Na Genofieva Matemu,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Serikali ya Tanzania kushirikiana na Wadau wa mchezo wa Riadha kuinua vipaji
Serikali
ya Tanzania kwa kushirikana na wadau wa mchezo wa riadha kutoka nchini
Italia imepania kuendeleza mchezo wa riadha ili kuinua vipaji vya
wanariadha chipukizi nchini.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel
wakati akiongea na Mkurugenzi wa Klabu ya Purosague Athelics ya Italia,
Bw. Nico Angelo Pannevis alipomtembelea ofisini kwake.
Prof
Gabriel amesema kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na Wadau wa
Mchezo wa Riadha ili kuhakikisha kuwa Wanamichezo chipukizi
wanaendelezwa na kufanya vizuri katika mashindano ya Kitaifa na
Kimataifa.
Naye
Bw.Pannevis ameeleza mpango wa Klabu yake wa kujenga kituo cha Mchezo
wa Riadha hapa nchini ili kuwaendeleza Wanariadha chipukizi katika
kuwajengea uwezo katika mchezo huo na fani nyingine za maisha.
Aidha,
Bw. Pannevis amesema kuwa hapo baadae Klabu yake haitajikita tu kwenye
riadha bali pia inalenga kuendeleza michezo ya walemavu ili kuwawezesha
kufikia ndoto zao za kimichezo kama wanamichezo wengine.
Alikiri kuwa Klabu yake imechagua kuendeleza michezo Tanzania ili kuitangaza Tanzania kupitia mashindano mbalimbali ya michezo ya Kimataifa.TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU UWE WA KWANZA KUPATA HABARI MOTOMOTO,PIA BOFYA HAYO MATANGAZO CHINI NA JUU KUJIFUNZA MAMBO MENGII(USIPITWEEE)
No comments:
Post a Comment