Meneja
Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bi. Badra Masoud
akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu taarifa za upotoshaji zilizotolewa
na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kwamba shirika hilo kuwa
hatarini kupelekwa mahakamani kufuatia kuvunja mkataba na kampuni ya
McDonald Live Line Technology Limited iliyoshindwa kutekeleza zabuni
iliyopewa kwa mujibu wa mkataba kati ya Pande hizo,kulia ni Afisa Habari
Idara ya Habari Maelezo bw. Frank Mvungi.
Shirika
la umeme Tanzania (TANESCO) Limekanusha taarifa iliyotolewa na baadhi
ya habari kuwa liko mbioni kufikishwa mahakama kutokana na kuvunja
mkataba na kampuni ya McDonald Live Line Technology Limited.
Akikanusha
taarifa hiyo Meneja Uhusiano wa shirika hilo Badra Masoud amesema kuwa
shirika liliamua kuvunja mkataba na kampuni hiyo baada ya kushindwa
kutekeleza zabuni waliyopewa ya kusafirisha, kusambaza na kuweka nguzo
za umeme katika eneo la Kiyungi/Arusha 06 kV lines iliyotakiwa
kukamilika ndani ya wiki 32 kuanzia Julai 28, 2010 na kuisha mwezi Machi
11, 2011.
Badra
aliongeza kuwa baada ya mkataba huo kuvunjwa kampuni ya McDonald
ilifungua shauri katika Tume ya Usuluhishi na Ushindani ambapo mara
baada ya pande zote kusikilizwa kampuni hiyo iliamriwa kuilipa TANESCO
fidia ya zaidi ya milioni 700.
No comments:
Post a Comment