Basi la kwanza la mradi wa mabasi
yaendayo haraka limewasili nchini na kuanza kufanya majaribio katika
barabara zilizokwisha kamilika huku mengine yakitarajiwa kuwasili mapema
mwaka kesho.
Mtendaji mkuu wakala wa mradi wa mabasi yaendayo haraka Bi Asteria
lambo amesema basi hilo ni miongoni mwa mabasi madogo yatakayoingia
nchini yenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 40 na makubwa yatabeba
abiria zaidi ya 150 na kuwataka wakazi wa jiji la Dar es Salamu
kuendelea kuwa na subira na kuwahakikishia mradi huo sio ndoto na adha
ya usafiri itapungua mapema mwaka kesho.
Nao baadhi ya wakazi wa jiji walioshuhudia gari hilo wameelezea
kufurahishwa na kuanza kuwa na imani na serikali yao ambapo wamesema
kama mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa utakuwa faraja sana
kutokana na adha kubwa ya usafiri wanayokumbana nayo huku wakitoa wito
kwa mamlaka husika kupanga mikakati ya kupunguza nauli za mabasi hayo
pindi yatakapoanza kufanya safari zao.
TUNAOMBA BOFYAHAPA LIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI NA ZA KUSISIMUAAA(USIPITWEEE)
TUNAOMBA BOFYAHAPA LIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI NA ZA KUSISIMUAAA(USIPITWEEE)
No comments:
Post a Comment